Madaktari bingwa waliofeli chuo Bugando wazua mjadala mtandaoni

November 4, 2021 12:55 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Wanafunzi 17 kati ya 19 wanaosemea udaktari bingwa wa magonjwa ya ndani wamefeli.
  • Baadhi ya watu wasema suala hilo linafikirisha.
  • Chuo chasema wasioridhishwa na matokeo hayo wakate rufaa.

Mwanza. Kufuatia wanafunzi wengi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Bugando (CUHAS) wanaosemea udaktari bingwa kufeli, uongozi wa chuo hicho umesema hayo ndiyo matokeo halisi na watu wako huru kutoa maoni kuhusu matokeo hayo.

Matokeo hayo yanawahusu wanafunzi wa mwaka wa pili wanaosemea udaktari bingwa wa magonjwa ya ndani (internal  medicine) wa mwaka 2021/22 ambapo kati ya watahiniwa 19 ni wawili tu ndiyo wamefaulu. 

Pia wanafunzi wa mwaka wa kwanza wanaosomea masomo hayo ni wawili kati ya nane tu ndiyo wamefaulu mitihani yao.

Kufuatia matokeo hayo, kumekuwa na mjadala mpana kwenye mitandao ya kijamii kuhusu matokeo hayo ikizingatiwa kuwa wanafunzi hao waliofeli ni madaktari waliofuzu na wameshafanya kazi kabla ya kwenda kusomea udaktari bingwa.

Mmoja wa watumiaji wa mtandao wa Instagram anayejulikana kwa malisa_gj amesema kuwa kama asilimia 87  wamefeli, tatizo haliwezi kuwa wanafunzi peke yao. Walimu ni tatizo pia.

“Kwanini vyuo vingine hawajafelisha kiasi hiki, ni Bugando tu?,  Kwanini haijawahi kutokea hivi miaka ya nyuma. Kwanini mwaka huu tu?,” amehoji mtumiaji huyo.

                                     

Mtumiaji mwingine wa Instragram, ikessy1, amesema “wani wahusika (waliofeli) wanasemaje? Hakuna utaratibu wa kulalamika kama wametendewa ndivyo sivyo? Na je ni lazima wafaulishwe hata kama wamefeli?”

Ameendelea kuuliza kuwa “lakini  pia udaktari bingwa ni kitu rahisi tu kupatikana? Tujiulize nchi ina madaktari bingwa wangapi kwa sasa au tangu Uhuru ili  kuona ilivyo rahisi au ngumu kuwapata.”

Kufuatia mjadala huo, uongozi wa chuo hicho umetoa ufafanuzi na kueleza kuwa matokeo hayo ni halisi na yalijadiliwa na kupitishwa na seneta ya chuo.

Makamu Mkuu wa hicho, Profesa Paschalis Rugarabamu amesema kuwa sheria, kanuni na taratibu za kuongoza chuo zinatoa nafasi kwa mtahiniwa ambaye hajaridhika na matokeo yake kukata rufaa.

“Kuhusu maoni ya jamii hatuna la kusema, watu na jamii wana haki na uhuru wa kutoa maoni yao,” amesema Prof Rugarabamu wakati akiongea na Nukta Habari (www.nukta.co.tz

Alipoulizwa maswali zaidi kama hawaoni kuwa matokeo hayo yanaharibu sifa ya chuo hasa ukizingatia waliofeli wametoka kwenye vituo vya kazi na wanatoa huduma kwenye jamii amesema suala hilo haliwezi kubadilisha ukweli kuhusu matokeo hayo.

 “Majibu yetu kwa mtu, chombo au mamlaka yoyote nje ya zile ambazo tunawajibika nazo moja kwa moja yanakomea katika jibu langu la mwisho. Nirudie kusema watu wako huru na wana haki ya kutoa maoni yao kadiri ya ufahamu wao,” amesema Prof Rugarabamu.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
24 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
24 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
24 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Baba Levo: Wazo la kuongeza tozo kwenye bodaboda litolewe, tuleteeni watu wa tungi

Baba Levo: Wazo la kuongeza tozo kwenye bodaboda litolewe, tuleteeni watu wa tungi

Nukta TV

Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Nukta TV

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Nukta TV