Fedha za IMF kupambana na Uviko-19 sekta ya maji Kagera
- Bodi ya IMF imeidhinisha mkopo wa Sh1.3 trilioni kuisaidia Tanzania katika kuhimili mahitaji yatokanayo na janga la Uviko-19.
Dar es Salaam. Shirika la Fedha Duniani (IMF) liliipatia Tanzania mkopo wa dharura wa Dola za Marekani milioni 567.25 (Sh1.3 trilioni) kwa ajili ya kukabiliana na athari za ugonjwa wa Corona (Uviko-19).
Taarifa ya IMF iliyotolewa Septemba 7 mwaka huu ilisema bodi ya shirika hilo imeidhinisha kutolewa kwa kiasi hicho cha fedha ambapo kitaisaidia Tanzania katika kuhimili mahitaji yatokanayo na janga la Uviko-19.
IMF ilieleza kuwa uchumi wa Tanzania ulitikisika kutokana na athari za Uviko-19, hivyo msaada wa kifedha ni muhimu kuurejesha katika hali ya kawaida.
Kati ya fedha hizo, Wizara ya Maji alipewa Sh139.4 bilioni ili kutekeleza miradi 218 katika Halmashauri mbalimbali ili kuboresha miundombinu ya maji ili kuwapunguzia wananchi makali ya Uviko-19 katika sekta ya maji.
Kati ya fedha hizo Mkoa wa Kagera umepata Sh2.94 bilioni kutekeleza miradi sita kama inavyoonekana katika infografia hii.

Latest
