Kinachofuata baada ya kirusi kipya cha Corona

December 7, 2021 2:31 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Inashauriwa kuendelea kutoa taarifa za ugonjwa huo kwa mamlaka za afya.
  • Watanzania wanashauriwa kuendelea kuchukua tahadhari.

Dar es Salaam. Endapo wewe ni mfuatiliaji mzuri wa habari, utakuwa umeshasikia juu ya aina mpya ya kirusi cha corona kilichogundulika nchini Afrika Kusini.

Kirusi hicho kilichopewa jina la Omicron kimeripotiwa kwa mara ya kwanza Novemba 24 katika nchi hiyo, miezi kadhaa baada ya kirusi cha Delta kutangazwa kutoka nchi hiyo hiyo.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kirusi hicho kinasambaa kwa haraka hivyo kinaweza kuwa na madhara makubwa kwa binadamu.

WHO imeshauri mamlaka za afya katika nchi mbalimbali kuchukua hatua za haraka dhidi ya Omicron ikiwemo kutoa taarifa juu ya ripoti za maambukizi zinazohusiana na kirusi hicho huku wananchi wakitakiwa kuendelea kuchukua tahadhari zote.

                           

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV