Wasifu wa video: Mbinu mpya ya waajiri kupata wafanyakazi

February 1, 2022 8:24 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Kampuni zinatumia njia hii kutafuta wafanyakazi wanaoweza kufanya kazi kidijitali.
  • Video za wasifu zinapima kujiamini, ubunifu na kumpa picha halisi mwajili.

Dar es Salaam. Hivi karibuni, nimekuwa nikifanya usajili wa kozi na fursa mbalimbali za kimataifa. Kati ya fursa tano nilizozichungulia, tatu zilikuwa zikihitaji wasifu wa video. 

Licha ya kuandika aya na aya za insha za kujibu maswali yaliyokuwa yameulizwa, swali la mwisho lilihitaji nirekodi video ili kujibu swali au kutoa  wasifu wangu.

Haiwezi kuwa bahati mbaya ya kuwa mashirika yote hayo yanahitaji video ya wasifu. Leo asubuhi pia, nimekutana na andiko la Mhariri wa Mtandao wa kijamii wa Linkedin, Gianna Prudente ambaye alikuwa akizungumzia hilo hilo.

Unaweza kurekodi video yako ukijielezea na kisha kuipakia kwenye mitandao kama Youtube, Linked in na kutuma kiunganishi kwa waajiri. Picha| The Balance Careers.

Sababu ya kufika huko

Teknolojia kwa sasa imeendelea na hauhitaji ofisi kufanya kazi. Unaweza kuwa na kompyuta yako na mtandao mzuri nyumbani na ukafanya kazi zako, ukahudhuria vikao vya kimataifa ndani ya nchi.

Mzalishaji wa maudhui ya mtandaoni kutoka Shirika la Habari la Uingereza (BBC) Casey Noenickx kupitia Linkedin amesema, ajira kwa sasa zinatolewa kwa njia ya mtandao hivyo wasifu wa video huenda ndiyo mwelekeo.

Noenickx amesema, “utafiti mmoja umeonyesha, asilimia 65 ya kampuni zimeajiri watu bila hata kuwahi kukutana nao.”

Hilo linaonyesha ya kuwa, huenda video za wasifu zikawa mbadala wa barua za maombi ya kazi katika siku za usoni.

Waajiri mbalimbali walioongea na BBC wamesema, wasifu wa video unaonyesha uhalisia wa mtu kuliko maandishi kwenye karatasi.


Soma zaidi


Wasifu wa video unaruhusu mwajiri kuchangamana na mwajiriwa na kupata mtazamo wa mtu na siyo maneno yaliyoandikwa.

Wasifu wa video unapima uwezo wa mtu kujieleza na pia kwa kazi zinazotafuta kujiamini, ubunifu na uwezo wa kujieleza, wasifu wa video ndiyo njia mpya ya kufikia baadhi ya kazi hizo.

Unasubiri nini? Tafuta kamera yako, eneo tulivu na rekodi video yako ya kujieleza. Huenda ukapata nafasi ya kazi ambayo imeombwa na wengi.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW