Mwendo wa kuperuzi: Watumiaji wa intaneti wazidi kuongezeka Tanzania

February 18, 2022 7:51 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Idadi ya Watanzania wanaotumia intaneti imeongezeka hadi kufikia milioni 29.8 mwaka 2021.

Dar es Salaam. Huenda idadi ya Watanzania wanaonufaika na fursa za mtandaoni imeongezeka, baada ya takwimu mpya za mawasiliano kuonyesha kuwa idadi ya Watanzania wanaotumia intaneti imeongezeka hadi kufikia milioni 29.8 mwaka 2021. 

Fursa zinazopatikana mtandaoni ni pamoja na biashara, ujuzi na maarifa yanayohitajika kuboresha maisha. 

Ripoti ya takwimu mpya za robo ya nne ya mwaka 2021 za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zilizotolewa hivi karibuni, zinaonyesha kuwa watumiaji wa intaneti wameongezeka hadi kufikia milioni 29.8 mwaka jana kutoka milioni 28.5 wa mwaka 2020. 

Hata hivyo, ripoti hiyo haijaweka wazi ni aina gani ya intaneti inayotumiwa zaidi na Watanzania kama ambavyo imekuwa ikifanyika miaka iliyopita, ambapo intaneti inayohamishika (mobile wireless) ambayo hutumika zaidi na simu za mkononi, tableti na kompyuta mpakato ndiyo imekuwa ikitumiwa zaidi na Watanzania.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
31 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
31 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV