Imenasa: Bei ya viazi mviringo Arusha yang’ang’ania pale pale

March 9, 2022 12:56 pm · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Bei ya juu ya gunia la kilo 100 la viazi mviringo linauzwa Sh80,000 katika mkoa huo, bei ambayo inafanana na ile iliyotumika ijumaa ya wiki iliyopita. 
  • Bei ya chini ni Sh53,000 ambayo nayo haijabadilika. 

Dar es Salaam. Bei ya jumla ya viazi mviringo katika Mkoa wa Arusha imeendelea kung’ang’ania kiwango kilekile cha Sh80,000 kilichorekodiwa Ijumaa Mei 22, 2020 jambo linalodhihirisha hakuna ongezeko la faida kwa wafanyabiashara mkoani humo. 

Takwimu za mazao makuu ya chakula zilizotolewa leo (Mei 29, 2020) na Wizara ya Viwanda na Biashara zinaonyesha gunia la kilo 100 la viazi mviringo linauzwa Sh80,000 katika mkoa huo, bei ambayo inafanana na ile iliyotumika Ijumaa ya wiki iliyopita.

Bei hiyo ndiyo bei ya juu kabisa huku bei ya chini ya zao hilo inayotumika leo mkoani humo ikiwa ni Sh75,000 ambapo nayo haijabadilika ukilinganisha na iliyorekodiwa wiki iliyopita. 

Hiyo ina maana kuwa wafanyabiashara wa zao hilo hawajaongeza faida ya zao hilo ndani ya wiki moja kwa sababu bei zimebaki zilizile, jambo ambalo pia ni ahueni kwa wanunuzi ambao wakati wote hupendelea bei ishuke.

Viazi mviringo ni miongoni mwa mazao ya chakula yanayotumiwa zaidi na Watanzania hasa kutengeneza chakula cha haraka kama chipsi. 

Hata hivyo, bei ya juu ya viazi mviringo inayotumika leo Tanzania Bara imerekodiwa katika mikoa ya Mwanza, Katavi, Morogoro, Tabora na Kagera ambapo gunia la kilo 100 linauzwa kwa Sh100,000 huku bei ya chini ni Sh53,000 ambayo imerekodiwa katika Mkoa wa Dodoma.

Enable Notifications OK No thanks