Wakulima, wafanyabiashara wa mahindi wazidi kuneemeka Tanzania

March 14, 2022 8:45 am · Herimina
Share
Tweet
Copy Link
  • Bei yapanda hadi Sh 65,864 Januari 2022 kutoka Sh56,866 ya Januari 2021. 
  • Bei ya mazao mengine makuu ya chakula nayo yapanda.
  •  Ogezeko la mahitaji ya zao hilo yachangia bei kupanda. 

Dar es Salaam. Neema yaendelea kuwashukia wakulima na wafanyabiashara wa mahindi, baada ya bei ya zao hilo kuendelea kupanda katika kipindi cha mwaka mmoja unaoishia Januari 2022.

Kwa mujibu wa ripoti ya mapitio ya uchumi kwa mwezi Februari 2022 (Monthly economic review) iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), bei ya jumla ya zao hilo (gunia la kilo 100) imeongezeka hadi kufikia Sh65,864 katika mwaka unaoishia Januari 2022 kutoka Sh56,866 iliyotumika kipindi kama hicho mwaka jana.

Hilo ni sawa na ongezeko la asilimia 13.7 au sawa na kusema wakulima wataweka kibindoni Sh8,997 kwa kila gunia la kilo 100 ambayo mwaka jana wasingeipata.

Hata hivyo, wanunuzi wa zao hilo watalazimika kutoboa zaidi mifuko yao na hivyo wanaweza kupata maumivu.

Mahindi ni miongoni mwa mazao makuu ya chakula yanayojumuisha mchele, maharage, viazi mviringo, mahindi, mtama, uwele na ulezi.

BoT katika ripoti hiyo imeeleza kuwa tangu Septemba 2021 bei ya mahindi imekuwa ikipanda kwa miezi minne mfululizo.

Ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa bei za mazao mengine ya chakula nazo zilipanda katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita isipokuwa maharage.

BoT inaeleza kuwa bei ya maharage iliyotumika mwaka unaoishia Januari 2022 ilikuwa Sh185,156 ikishuka kutoka Sh198,531 iliyotumika katika kipindi kama hicho mwaka jana. 

BoT imeeleza kuwa sababu ya kupanda kwa bei ya mazao ya chakula ni kuongezeka kwa uhitaji wa mazao hayo sokoni hasa kipindi hiki ambacho wakulima wanapanda mazao yao. 


Soma zaidi:


Wakati bei za mazao makuu ya chakula zikipanda, pia akiba ya chakula katika Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) imeongezeka na kufikia tani 207,899 mwaka unaoishia Januari 2022 kutoka Sh110,398 kipindi kama hicho mwaka jana. 

Hat hivyo, katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, akiba ya chakula cha NFRA imekuwa ikipanda na kushuka.

Mathalan, mwezi Desemba wakala huo ulikuwa na akiba ya tani 214,968 ambayo ndiyo kiwango cha juu kabisa ndani ya mwaka mmoja uliopita ambapo imeshuka hadi tani 207,899 Januari 2022.

Ripoti ya BoT inaeleza kuwa mwezi Januari 2022, NFRA ilinunua tani 196.5 za mahindi kutoka kwa wakulima na wafanyabiashara wa ndani ya na kuuza tani 7,265.9 za zao hilo.

Hatua hiyo ilichangia kupungua kwa akiba ya chakula katika maghala yake kwa mwezi Januari 2022.

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV