Waziri Ummy: Kirusi kipya cha Uviko-19 hakijafika Tanzania

March 23, 2022 12:24 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Asema kwa sasa wanapambana na kirusi cha Omicron.
  • Baadhi ya nchi zaripoti kirusi hicho chenye muunganiko wa Delta na Omicron.
  • Tanzania yaendelea kutoa chanjo. 

Dar es Salaam. Wakati Serikali ya Tanzania ikiendelea na zoezi la utoaji chanjo dhidi ya virusi vya Corona (Uviko-19), imesema kirusi kipya cha ugonjwa huo ambacho kimeripotiwa katika baadhi ya nchi duniani hakijafika bado Tanzania. 

Waziri wa Afya Umri Mwalimu aliyekuwa akizingumza leo Machi 23, 2022 wakati akipokea dozi milioni 1 za chanjo aina ya Sinovac, msaada kutoka Uturuki amesema taarifa zilizopo katika wizara yake hadi leo asubuhi ni kuwa hakuna kirusi kipya kilichoripotiwa nchini zaidi ya kirusi aina ya Omicron. 

“Asubuhi nilikuwa naongea na Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu hicho kirusi kipya wakaniambia bado wanaendelea kufanya tafiti kujua kitakuwa kikali kiasi gani na madhara yake yatakuwaje. Habari njema ni kwamba na sampuli nilizoelekeza zichukuliwe kuangalia kama tuna kirusi hicho zimeoonyesha hatuna bado tuna Omicron,” amesema Ummy.

Kwa mujibu wa WHO, baadhi ya nchi zimeanza kuripoti uwepo wa kirusi hicho kipya kinachodaiwa kuwa na muunganiko wa Delta na Omicron.


Zinazohusiana


Utoaji wa chanjo

Aidha, amesema hadi kufikia Machi 21, 2022 jumla ya watu milioni 3.01 wamepata chanjo kamili kati ya watu milioni 30.7 wenye umri wa miaka 18 na kuendelea ikiwa ni sawa na asilimia 9.81.


“Nachukua fursa hii kuendelea kuwasisitiza viongozi na watendaji wa ngazi zote kuendelea kutoa ushirikiano ili wananchi waendelee kuhimizwa kupata elimu ya chanjo ili wapate chanjo wajikinge na maambukizi ya Uviko-19,” amesema Ummy.

Waziri Ummy amesema Serikali inalenga kuchanja asilimia 70 ya Watanzania kuanzia umri wa miaka 18 hadi mwisho wa mwaka 2022.

Wananchi wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari zote ikiwemo kunawa mikono, kuvaa barakoa, kutumia vitakasa mikono na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima.

/
No matches found for this filter
30 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
30 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
30 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV