Kifua kikuu bado tishio kwa afya za Watanzania

March 24, 2022 7:20 am · Herimina
Share
Tweet
Copy Link
  • Mwaka 2021 kulikuwa na wagonjwa wa kifua kikuu takriban 133,000 nchini.
  • Tanzania ni miongoni mwa nchi 30 duniani zenye tatizo kubwa la ugonjwa huo.
  • Elimu na kuimarisha matibabu kunaweza kupunguza tatizo.

Dar es Salaam. Licha ya Tanzania kuimarisha matibabu ya kifua kikuu (TB), imetajwa kuwa miongoni mwa nchi 30 duniani ambazo watu wake wanateswa zaidi na ugonjwa huo, Shirika la Afya Duniani (WHO) linaeleza.

Kwa mujibu wa WHO, mwaka 2021 kulikuwa na wagonjwa wa kifua kikuu takriban 133,000 nchini.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, ugonjwa wa kifua kikuu unawaua watu wengi zaidi kuliko ugonjwa mwingine wowote ule wa kuambukiza ambapo watu milioni 1.5 walikufa kutokana na ugonjwa huo mwaka 2018. 

WHO inaeleza kuwa Karibu watu milioni 10 wanaambukizwa kifua kikuu kila mwaka na idadi ndogo tu ya visa hivyo wanapatiwa dawa muhimu za kuokoa maisha huku zaidi ya watu 4,000 wanakufa kwa kifua kikuu kila siku duniani.

 Takwimu hizo zimetoka ili kutoa fursa kwa Serikali na jamii kutafuta namna ya kukabiliana na ugonjwa huo wakati leo Machi 24, 2022 dunia akiadhimisha Siku ya Kifua Kikuu, lengo likiwa ni kuleta hamasa na kutoa elimu kwa jamii juu ya ugonjwa huo, na kwa Tanzania mwaka huu maadhimisho hayo yanafanyika Mkoa wa Tanga katika viwanja vya Tangamano.

Kifua kikuu ni chanzo kikubwa cha vifo miongoni mwa wanaoishi na virusi vya Ukimwi (VVU). 


Zinazohusiana:


Kutokana na athari za ugonjwa huo, Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-Tamisemi na wadau wanaotekeleza kazi za kifua kikuu wanaitumia siku ya leo kutoa elimu na hamasa kwa umma, uchunguzi na upimaji wa kifua kikuu pamoja na kuanzisha matibabu kwa wagonjwa watakaobainika kuwa na maambukizi.

Kituo cha Kudhibiti Magonjwa cha Marekani (CDC) ni moja ya wadau ambao wameendelea kutoa huduma jumuishi za VVU na kifua kikuu katika mikoa 11 ya Tanzania bara na Zanzibar.

Huduma hizo ni pamoja na uwezo wa maabara kutambua magonjwa, uchunguzi wa kifua kikuu, vituo vya huduma, kinga kwa watu wanaoishi na VVU na ufuatiliaji wa upinzani wa dawa za kifua kikuu.

Kituo hiki kimesaidia kuongeza kiwango cha tiba kinga kutoka asilimia 6 mwaka 2019 hadi asilimia 72 mwaka 2021 na kinatumia teknolojia mpya ili kuboresha matokeo ya wagonjwa kuweza kudhibiti na kukomesha kifua kikuu.

Aidha, Wizara ya Afya inahimiza jamii kujitahadharisha na mambo yanayochochea kuenea kwa ugonjwa wa kifua kikuu ikiwa ni pamoja na misongamano, lishe dunii, matumizi ya tumbaku, unyafuzi kwa watoto na maambukizi ya VVU.

/
No matches found for this filter
26 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
26 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: KOMBO AKIWASILISHA BAJETI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE BUNGENI 2026/2027

🔴LIVE: KOMBO AKIWASILISHA BAJETI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE BUNGENI 2026/2027

Nukta TV

JINSI WAHAMIAJI HARAMU WANAVYOONGEZEKA TANZANIA

JINSI WAHAMIAJI HARAMU WANAVYOONGEZEKA TANZANIA

Nukta TV

VIJANA WA TANZANIA KUNUFAIKA NA UCHUMI WA KIDIGITALI

VIJANA WA TANZANIA KUNUFAIKA NA UCHUMI WA KIDIGITALI

Nukta TV