Nishati ya jotoardhi itakavyomaliza tatizo la umeme Tanzania

November 25, 2022 1:35 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Nishati hiyo iliyopo nchini inaweza kuzalisha umeme wa megawati 5,000.
  • Mikoa 16 ina rasilimali hiyo ikiwemo Mbeya
  • Ikiwa itatumiwa vizuri itasaidia kuondoa tatizo la umeme. 

Dar es Salaam. Huenda tatizo la kukatika kwa umeme likamalizika nchini mara baada ya kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) kuanza  utekelezaji wa miradi mitano ya kipaumbele ya rasilimali ya jotoardhi itakayoongeza upatikanaji wa nishati hiyo nchini. 

Kampuni   hiyo  ni kampuni tanzu  ya Shirika  la umeme Tanesco ambapo inatekeleza nishati  ya jotoardhi  inayochimbwa urefu wa kilometa  tatu kwenda chini na  ambapo rasilimali zilizopo zinaweza kuzalisha umeme wa megawati  5,000. 

Kaimu Meneja Mkuu wa  kampuni ya TGDC, Mhandisi Shakiru Kajugus alikuwa akizungumza hivi karibuni  katika ziara ya Bodi ya Wakurugenzi ya kampuni hiyo ilipotembelea  eneo la mradi lililipo  Ziwa Natron wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

 Amesema kuwa, nishati hiyo ya jotoardhi inapatikana kwa wingi katika maeneo ya bonde la ufa ambapo kwa upande wa  Ziwa Natron wapo katika hatua za utafiti kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo ambao utazalisha megawati  60 na unatarajiwa kukamilika  mwaka  2025 .

“Mradi huu wa Ziwa Natron kwa kuanzia tutazalisha megawati 10 baada ya hapo tunaendelea na upanuzi zaidi na unatarajiwa kugharimu  kiasi cha zaidi ya  Sh1 bilioni  na kukamilika kwa mradi huo  kutaleta manufaa makubwa sana kwa wananchi kwani ni nishati endelevu ya kisasa isiyotegemea mabadiliko ya tabianchi,” amesema Mhandisi Kajugus.

Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya kampuni ya TGDC wakikagua mradi wa jotoardhi uliopo Mkoa wa Manyara. Picha | TGDC/Instagram.

Tanzania kwa sasa inatekeleza miradi mitano ya kipaumbele ya joto ardhi  Wilaya ya Rungwe katika maeneo ya  Ngozi  na Kiejo – Mbaka mkoani Mbeya.

Mikoa mingine ni Songwe na Pwani na tayari  ipo katika hatua ya uhakiki kwa ajili ya kuchimba visima huku kwa mkoa wa Arusha wakiendelea  na tafiti za kisayansi ambazo zinatarajiwa kumalizika mwaka 2023.

Nishati ya jotoardhi ina matumizi mengi ikiwemo kuzalisha umeme ambao hutumika kuendeshea mitambo, kupikia na kutoa mwanga majumbani.

Mwenyekiti wa bodi ya TGDC, Profesa Shubi Kaijage amesema bodi mpya wamefikia hatua ya kutembelea  moja ya miradi ya jotoardhi kujionea  na kuweza kuangalia cha  kushauri  ili mradi huo uweze  kufanyiwa kazi kwa haraka na kwa weledi.

Amesema kuwa, nishati hiyo inapatikana chini ya ardhi kwa kutumia joto lililopo  chini ya ardhi na kuwa itaweza kupunguza changamoto ya mgao wa umeme uliopo hivi sasa unaosababishwa na ukame.

“Sisi kama bodi tunaendelea kuhakikisha tunasimamia kikamilifu mradi huu ili uweze kukamilika kwa wakati na tunaomba kampuni hii iendelee kutekeleza majukumu  yake kwa wakati ili tuendelee kupata vyanzo   zaidi vya umeme,” amesema Prof Kaijage. 

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
25 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV