Rugambwa asimikwa rasmi kuwa Kardinali, Tanzania sasa kupiga kura mbili uchaguzi wa Papa

October 1, 2023 11:04 am · Daniel
Share
Tweet
Copy Link
  • Anakuwa kardinali watatu kutoka Tanzania.
  • Amesimikwa pamoja na wengine 20 kutoka nchi 11, tatu zikiwa za Afrika Tanzania, Nigeria na Sudan. 

Dar es Salaam. Hatimaye Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu la Tabora Protase  Rugambwa, amesimikwa rasmi hii leo na Papa kuwa Kardinali kufuatia uteuzi wake wa Julai 10, 2023.

Mwadhama Kardinali Rugambwa amesimikwa sambamba na  wengine 20 kutoka nchi 11 tatu zikiwa za Afrika ambazo ni Tanzania, Sudani ya Kusini na Afrika kusini katika kanisa la Mtakatifu Petro, Vatican ambapo 20 kati yao ni maaskofu na mmoja ni padre.

Rugambwa ambaye aliteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Tabora Aprili, 2023 anakuwa kardinali watatu kutoka Tanzania, akitanguliwa Kardinali wa kwanza Laurean Rugambwa ambaye hakuwa sio tu alikuwa mtanzania wa kwanza kushika nafasi hiyo bali ndiye mwafrika wa kwanza kuteuliwa kuwa kardinali.

Mwadhama Laurean Kardinali Rugambwa alifuatiwa na Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo ambaye aliteuliwa na Papa Yohan Paul wa II tarehe 21 Februari 1998, hadi sasa ambapo amestafuu kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam.

Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa sasa anaingia katika kundi la makardinali ambao watakuwa na uwezo wa kuchagua mrithi wa Papa Francis katika kikao cha siri cha kipapa baada ya kifo chake au kujiuzulu, ambapo  kwa mujibu wa sheria za kanisa Kardinali mwenye umri miaka 80 harusiwi kupiga kura.

Soma zaidi:

Kardinali ni nani?

Kardinali ni nyazifa ya pili ya kwa ukubwa katika muundo wa Kanisa Katoliki  baada  ya Papa.

Aidha, wanatumika kama washauri wake wa karibu kuhusu masuala ya mafundisho na utawala. Ingawa,  wajibu wao muhimu zaidi ni kukutana katika kikao cha siri kuchagua Pontifex mpya kwa mujibu wa sheria za kanisa (Canon law 349).

Kutokana na nguvu na ushawishi wao wa kihistoria, bado wanaitwa ‘The Princes of the Church’.

Licha ya upekee huo Papa Francis amewahi kuwasi kutokuishi kama wafalme bali kuwa karibu na masikini.

           

           

 

Kabla ya kusimikwa kwa makardinali wapya leo kulikuwa na makadinali 221 ulimwenguni huku makadinali 119 tu ndio walikuwa na uwezo wa kupiga kura ya kumchagua Papa huku  Polycarp Kardinali Pengo kutoka Tanzania akiwemo.

Katika uteuzi huu wa Papa Francis wa makadinali 21 ni 18 ndio wata kuwa na  uwezo wa kupiga kura hivyo kufanya kuanzia leo kuwa jumla ya makadinali 242 ambapo kati yao 121 ndio wana  uwezo wa kupiga kura.

Hiyo inaifanya Tanzania kuwa miongoni wa nchi mbili Afrika ikiwemo Nigeria zeye makadinali wawili wenye uwezo wa kupiga kura akiwamo Protase Rugambwa.

Uteuzi wa Papa Francis unafanya kuwa na jumla ya makadirnali 121 kutoka katika nchi 66 duniani ambao ni sawa na asilimia 55 ya makadinali wote wenye  uwezo wa kupiga kura huku wale waliochaguliwa na Papa Francis pekee  na wana uwezo wa kupiga kura ni 98 ambapo ni sawa na asilimia 72.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW