Zingatia haya kuepuka magonjwa unaposafiri nje ya nchi
- Ni pamoja na kung’atwa na wadudu wanaoweza kukupa magonjwa.
- Inashauriwa kuwa na uhakika na wa chakula unachokula.
- Tumia mafuta maalumu kujikinga na mionzi ya jua.
Safari za nje ya nchi ni raha kwani unapata nafasi ya kukutana na tamaduni mpya na hata watu wenye hulka ya tofauti na yako.
Mwaka 2022 unaweza kuwa mwaka wako wa kusafiri nje ya nchi ili kuzifikia ndoto zako ikiwemo kwenda kusoma, kutalii au kufanya biashara.
Kusafiri nje ya nchi kunaweza kuwa kwa usafiri ndege, meli, gari na hata treni.
Kabla haujaingia kwenye sintofahamu ya maradhi yanayoweza kukupata ukiwa safarini, ni vyema ukafahamu mambo muhimu kujiweka salama wakati wa safari yako:
Wadudu wa kung’ata
Wakati wadudu wengine wanaweza kukupatia muwasho wa kawaida, wengine wanaweza kukulaza kitandani kwa ugonjwa.
Mbu, mbung’o, viwavi na wadudu wengine wanatofautina kutoka nchi na nchi.Â
Inashauriwa kubeba dawa za kufukuza wadudu (repellants) na ujue muda gani wadudu wanafanya kazi zaidi.
Kati ya vitu muhimu kwa wewe kubeba, ni dawa za kufukuza wadudu. Picha| CDC.
Chakula kisichokufaa
Safari huambatana na utafiti wa kujua tamaduni za huko unakoenda. Kuanzia chakula, mavazi na mtindo wa maisha.
Kuwa makini. Huenda tumbo lako lisiwe tayari kwa baadhi ya vyakula ambavyo utataka kuvionja.
Iwe ni matunda, nyama choma na vyakula vingine, penda kuuliza kabla ya kuamua kuvitumia.
Soma zaidi
- Mambo 10 ya kuyafahamu kabla ya kuanza kufuga kasuku
- Mambo muhimu ya kuzingatia kabla, baada ya kununua kondomu
- Ufahamu mlima uliotengenezwa kwa taka za kielektroniki
Hali ya hewa
Kila nchi na hali yake ya hewa. Wakati umetoka kwenye nchi yako ya baridi, huenda uendako kuna joto la ajabu. Ni kama mtu wa Mbeya anavyolalamika akifika Dar es Salaam.
Hakikisha unafahamu hali ya hewa ya huko uendako itakusaidia kuchagua mavazi sahihi na kujua kama utahitaji mafuta kwa ajili ya kukuepusha na mionzi ya jua (sunburn).
Mambo hayo yanaweza kukusaidia wakati ukisafiri. Tuambie ni mambo gani ambayo unafikiri ni muhimu kuzingatia unaposafiri nje ya nchi?