Wizara ya Elimu yatangaza ufadhili diploma ya ualimu makundi maalumu

August 20, 2025 12:51 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Maombi yatapokelewa kwa siku 15 kuanzia Agosti 18 hadi 28, 2025.
  • Wanufaika ni wanafunzi wa shahada ya elimu maalum.    

Arusha. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetangaza fursa ya ufadhili wa masomo ya elimu ya juu kwa ngazi stashahada ya ualimu wa elimu ya juu kwa miaka miwili.

Taarifa ya Prof.Carolyne Nombo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo iliyotolewa Agosti 20, 2025 inabainisha kuwa maombi yatakayopokelewa kwa ajili ya ufadhili huo ni kwa wanachuo wanaosoma stashahada ya elimu maalumu katika maeneo  ya ulemavu wa akili, usonji, uziwi, na ulemavu wa uoni.

Miongoni mwa sifa za msingi zilizoanishwa na Wizara hiyo ni kuwa Mtanzania pamoja na kudahiliwa chuo cha ualimu kinachotambulika na Serikali kinatoa Stashahada ya Ualimu Elimu Maalumu.

“Nakala za kuwasilisha ni barua ya kuomba ufadhili ikionesha kozi unayosoma, namba ya simu na barua pepe, nakala ya vyeti vya kitaaluma vilivyothibitishwa na mwanasheria, cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na mwanasheria na barua kutoka kwa mkuu wa chuo ikionesha kuwa umedahiliwa katika chuo husika,” imebainisha taarifa ya Nombo.

Aidha, Wizara hiyo imebainisha kuwa ufadhili huo utahusisha mahitaji mbalimbali ikiwemo ada ya mafunzo miichango mingine ya chuo (kama  ulinzi, ukarabati), vifaa vya kufundishia na kujifunzia, nauli na  bima ya Afya.

Masharti ya ufadhili

Wizara ya Elimu imesema miongoni mwa masharti muhimu ya kupata ufadhili huo ni pamoja na  kusoma, kuelewa na kusaini mkataba wa makubaliano ya ufadhili wa masomo kati yake na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na kuwa na akaunti ya benki kwa ajili ya fedha atakazolipwa moja kwa moja.

“Mnufaika hataruhusiwa kubadilisha programu ya masomo aliyopatia ufadhili bila idhini ya Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, mnufaika hataruhusiwa kuahirisha masomo, isipokuwa kwa sababu za kiafya, na kuthibitishwa na Daktari kutoka katika Kituo cha Afya au Hospitali inayotambuklika na Serikali,” imeongeza wizara hiyo.

Ikiwa mnufaika ataghairi fursa ya ufadhili, atapaswa kutoa taarifa kwa maandishi kwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia kwa Mkuu wa chuo alichodahiliwa na kujisajili.

Taarifa ya Nombo imebainisha kuwa maombi ya ufadhili huo yanatakiwa kuwasilishwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ndani ya siku 15 kuanzia Agosti 18 hadi 28, 2025. 

Maombi hayo pia yanaweza kutumwa kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia sanduku la Posta S.L.P 10 Dodoma na rodha ya Wanachuo watakaokuwa wamepata ufadhili huo itawekwa katika tovuti ya Wizara (www.moe.go.tz).

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
21 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
21 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
21 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Nukta TV

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Nukta TV

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

Nukta TV