William Lukuvi afariki dunia

March 25, 2026 10:13 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Amefariki dunia katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, Jijini Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa mshtuko wa moyo.

Arusha. Aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) na Mbunge wa Jimbo la Isimani (CCM), William Vangimembe Lukuvi amefariki dunia leo Machi 25, 2026, majira ya saa moja asubuhi kutokana na mshtuko wa moyo.

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo cha mbunge huyo kupitia taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dk Moses Kusiluka iliyotolewa leo Machi 25, 2025 ikifafanua kuwa Lukuvi amefariki dunia katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, Jijini Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa mshtuko wa moyo.

Kufuatia msiba huo, Rais Samia ametoa pole kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, familia, wananchi wa Jimbo la Isimani, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote.

Lukuvi (70) amepoteza maisha ikiwa ni takribani miezi minne tangu apewe ridhaa ya kuongoza Jimbo la Isimani lililopo mkoani Iringa, akiteuliwa pia kuiongoza Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu).

Kiongozi huyo ambaye ni miongoni mwa viongozi wakongwe zaidi nchini Tanzania akiwa na zaidi ya miaka 30 Bungeni atakumbukwa kwa utendaji kazi wake na ufanisi katika siasa ulimuwezesha kuwapika wanasiasa wachanga.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
26 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Lissu alivyotumia saa tisa kujitete mahakamani, aibua hoja tatu nzito

Lissu alivyotumia saa tisa kujitete mahakamani, aibua hoja tatu nzito

Nukta TV

Walimbwende ‘Miss World’, kupewa makabila Tanzania kuwakilisha kimataifa

Walimbwende ‘Miss World’, kupewa makabila Tanzania kuwakilisha kimataifa

Nukta TV

Makonda: Jezi ya Taifa Stars mbaya, hangaikeni  iwe nzuri

Makonda: Jezi ya Taifa Stars mbaya, hangaikeni iwe nzuri

Nukta TV