WhatsApp kuachana na baadhi ya simu za Iphone, android

May 15, 2019 8:58 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Hatua hiyo ni kujihakikishia usalama wa huduma inazotoa kwa watumiaji wa mtandao huo. Picha|Mtandao.


  • Inakusudia kujitoa na kutopatikana katika baadhi ya simu zinazotumia programu endeshi za windows ifika mwishoni mwa mwaka huu. 
  • Pia itajiondoa katika simu za Iphone IOS 7 na Android toleo la 2.3.7  ambapo mwisho  wa kutumika itakuwa Februari 1, 2020.
  • Hatua hiyo ni jitihada za kujihakikishia usalama mtandaoni.

Dar es Salaam.Mtandao wa kijamii wa WhatsApp umetoa angalizo kwa watumiaji wake kuwa  ifikapo mwanzoni mwa mwaka 2020 haitakuwa inapatikana katika baadhi ya matoleo ya simu za mkononi ikiwemo zinazotumia programu endeshi ya ‘windows’

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mtandao huo wenye watumiaji zaidi ya bilioni 1.5, huduma zake hazitapatikana katika simu zinazotumia programu ya window ifikapo Disemba 2019.

Angalizo hilo pia linawahusu wamiliki wa simu za Iphone toleo la IOS 7 na matoleo yote yaliyotengenezwa nyuma na simu zinazoendeshwa na programu ya Android toleo la  2.3.7 (Android versions 2.3.7) na matoleo yote ya nyuma ambapo kwa pamoja zitafikia ukomo wa matumizi ifikapo Februar 1, 2020.

“kwa simu zinazotumia toleo la androdi 2,3,7 na nyuma ya hapo mtumiaji wake hataweza kufungua akaunti mpya wala kuthitisha akaunti zake zilizofunguliwa tayari, lakini wataendelea kutumia WhatsApp mpaka Februari 1, 2020,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.


Zinazohusiana: 


WhatsApp imechukua uamuzi huo ikiwa ni hatua ya kuendana na mabadiliko ya teknolojia ya simu za kisasa ikizingatia kuwa matoleo yaliyotajwa hapo juu yanakabiliwa na changamoto ya masasisho ya teknolojia na idadi ya watumiaji wake inapungua kwa kasi. 

Lakini sababu nyingine ni kuiweka WhatsApp katika programu za simu zenye usalama zaidi na kuepusha na udukuzi wa taarifa za watumiaji wake.

Siyo mara ya kwanza kwa mtandao huo kujitoa katika baadhi ya matoleo ya simu, ilifanya hivyo mwaka 2017 ambapo haipatikani tena katika matoleo ya simu za Nokia Symbian S60 na Black Berry OS ambapo mwaka jana ilijitoa katika simu ya Nokia S40.

Enable Notifications OK No thanks