Watumiaji wa Facebook, Instagram kuongezewa ulinzi
- Ni kupitia marekebisho ya mpangilio wa usimbaji fiche (end-to-end encryption).
- Kipengele hicho kitakuwa cha lazima kwa watumiaji wote.
- Itasaidia kupunguza udukuzi na kuingilia faragha za watumiaji.
Kampuni ya Meta inafanyia marekebisho ya mpangilio wa usimbaji fiche (end-to-end encryption) kwenye program zake za mawasiliano ili kuongeza usalama na ulinzi wa faragha za watumiaji wote.
Usimbaji fiche (End-to-end encryption) ni njia ya kuwasiliana kwa usalama ambayo inahakikisha watu wanaowasiliana au kutumiana ujumbe ndiyo wanaoweza kuona maudhui yao bila kuingiliwa na mtu wa tatu.
Meta imeelaza hayo August 11, 2022 California nchini Marekani kuwa inaanza majaribio ya mpangilio wa usimbaji fiche kwenye program zake ya kutuma na kupokea jumbe (Messenger) lengo likiwa ni kuboresha usalama wa taarifa za watumiaji.
Uboreshaji huu ni baada ya Facebook kukabiliwa na kashfa kwa kufichua mazungumzo ya faragha kwa polisi wanaochunguza madai ya utoaji mimba kinyume cha sheria katika jimbo la Nebraska nchini Marekani.
“Tunajaribu uhifadhi salama kwenye Messenger, kipengele kipya kinachokuruhusu kuhifadhi nakala za chati zako zilizosimbwa kwa njia fiche kutoka mwanzo hadi mwisho (end-to-end encryption),” imeeleza Meta kupitia tovuti yake.
Kwa sasa Facebook inaruhusu watumiaji kuchagua mpangilio huo kwa hiari, ila marekebisho mapya yamelenga kufanya mpangilio huo kuwa wa lazima kwenye Messenger.
Soma zaidi:
Majaribio ya uboreshaji faragha hiyo yalianza mwaka jana kwa baadhi ya watumiaji, ila sasa yemelengwa kutumika kwa watumiaji wote.
“Pia tunaanza jaribio la mazungumzo ya kiotomatiki yaliyosimbwa kutoka mwisho hadi mwisho kwenye Messenger na kupanua vipengele vingine.” iliongeza Meta ili kuleta matumizi bora zaidi kwenye Messenger na Instagram.
Hata hivyo, maboresho hayo yanategemewa kukamilika mwakani kwenye programu za jumbe za mitandao ya kijamii ya Facebook na Instagram.
Sara Su ambaye ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa Bidhaa za Meta huku amesisitiza kuwa, wataendelea kutoa masasisho (updates) kuelekea usambazaji wa kimataifa wa usimbaji fiche wa ujumbe wa binafsi na simu mnamo 2023.
Latest
