Watahiniwa kidato cha pili waanza mitihani leo, kidato cha nne wakiendelea

November 11, 2019 8:35 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link

Katika matokeo ya mwaka jana 2018, jumla ya wanafunzi 545,077 walisajiliwa kufanya mtihani wa kitaifa wa kidato cha pili (FTNA) mwaka 2018, ambapo  wanafunzi 506,235 ndiyo walifanya mtihani huo. Picha|Mtandao.


  • Watahiniwa 602,502 wamesajiliwa kufanya mitihani hiyo kwa mwaka 2019.
  •  Mitihani ya upimaji kwa darasa la nne nayo kufanyika Novemba 20 na 21, mwaka huu. 
  • Necta imetoa wito kwa kamati mbalimbali kuhakikisha taratibu zote za mitihanii zinafuatwa ipasavyo.

Dar es salaam. Wakati watahiniwa kidato cha nne nchini Tanzania wakiendelea na mitihani, wenzao wa kidato cha pili wameanza mitihani yao leo katika maeneo mbalimbali nchini.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde amesema mitihani hiyo iliyoanza leo ifanyika mpaka Novemba 22, 2019 ikiwa ni mtihani wa upimaji kidato cha pili katika elimu ya sekondari. 

Dk Msonde aliyekuwa akizungumza na wanahabari jana amesema jumla ya watahiniwa 602,502 kutoka shule 4,796 wamesajiliwa kufanya mtihani huo kwa mwaka huu.

Hilo ni ongezeko la watahiniwa 64,636 sawa na asilimia 11.86 ikilinganishwa na mwaka 2018.

Dk Msonde amezitaka  kamati zote za mitihani za mikoa, halmashauri, manispaa na majiji kuhakikisha taratibu za mitihani zinafuatwa ipasavyo ili kuepuka vitendo vya udanganyifu na wizi wa mitihani. 

“Baraza linapenda kutumia nafasi hii kutoa wito kwa kamati zetu zote za uendeshaji wa mitihani za mikoa pamoja na halmashauri katika Taifa letu. Kamati zihakikishe kuwa taratibu zote za uendeshaji upimaji huu wa mitihani ya Taifa zinazingatiwa ipasavyo,” amesema Dk Msonde.

Katika matokeo ya mwaka jana 2018, jumla ya wanafunzi 545,077 walisajiliwa kufanya mtihani wa kitaifa wa kidato cha pili (FTNA) mwaka 2018, ambapo  wanafunzi 506,235 ndiyo walifanya mtihani huo. 

Kati ya idadi hiyo, wanafunzi 52,273 sawa na asilimia 89.68 waliofanya mtihani huo walifaulu kuendelea na masomo ya kidato cha tatu. Katika mtihani wa mwaka huu, ufaulu utapanda au kushuka?


Zinazohusiana:


Katika hatua nyingine, ametangaza kuanza kwa mitihani ya upimaji kwa darasa la nne itakayofanyika Novemba 20 na 21, 2019 wakati mithihani ya kidato cha pili ikiendelea.

Katika mitihani hiyo ya upimaji darasa la nne, idadi ya watahiniwa imeongezeka kwa asilimia 53.96 hadi kufikia milioni  1.7  kutoka milioni 1.2 walioandikishwa kufanya mtihani huo mwaka jana.

Kwa muktadha huo, mwezi huu wa Novemba Tanzania inashuhudia mitihani mitatu ngazi ya Taifa ya kidato cha pili, nne na ule wa darasa la nne.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV