Watahiniwa 14 wafutiwa matokeo mtihani kidato cha sita 2019

July 11, 2019 10:47 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Wamefutiwa matokeo hayo baada ya kubainika kuwa walifanya udanganyifu.
  • Tisa ni watahiniwa wa shule na watano ni watahiniwa wa kujitegemea. 
  • Watahiniwa 20 matokeo yao yamezuiliwa baada ya kupata matatizo ya kiafya.

Dar es Salaam. Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) limefuta matokeo ya watahiniwa 14 waliobainika kufanya udanganyifu katika mitihani ya kidato cha sita uliofanyika Mei mwaka huu. 

Licha ya vitendo hivyo vya udanganyifu, ufaulu wa jumla wa katika mitihani hiyo umeongezeka kwa asilimia 0.74 kutoka asilimia 97.58 mwaka 2018  hadi asilmia 98.32  mwaka huu.

Katibu Mkuu wa Necta, Dk Charles Msonde aliyekuwa akitangaza matokeo hayo leo (Julai 11, 2019) Unguja, Visiwani Zanzibar amesema kati ya watahiniwa hao waliofutiwa matokeo, tisa ni watahiniwa wa shule na watano ni watahiniwa wa kujitegemea. 

“Baraza la Mitihani la Tanzania limefuta matokeo yote ya watahiniwa 14 waliobainika kufanya udanganyifu katika mtihani,” amesema Dk Msonde. 

Idadi ya watahiniwa waliofutiwa matokeo  mwaka huu imeongezeka ikilinganishwa na mwaka jana ambapo waliofutiwa matokeo kwa kuhusika na udangajifu walikuwa nane tu. 

Hata hivyo, Dk Msonde hajawataja watahiniwa waliofutiwa matokeo, wala shule wanazotoka.


Soma zaidi: Ufaulu kidato cha sita waongezeka kwa asilimia 0.74


Katika hatua nyingine, Necta imezuia kutoa matokeo ya watahiniwa 20 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mtihani kwa baadhi ya masomo. 

“Watahiniwa husika wamepewa fursa ya kufanya mtihani wa kidato cha sita Mei, 2020 kama watahiniwa wa shule,” amesema Dk Msonde. 

Amebainisha kuwa licha ya kubainika kwa vitendo hivyo vya udangajifu, wasimamizi wa mitihani walifanya kazi kubwa ya kudhibiti vitendo hivyo visitokee kwa kuzingatia taratibu zote zilizowekwa na baraza hilo. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴 LIVE: WABUNGE WAKIMCHAPA MASWALI MAZITO WAZIRI MKUU BUNGENI

🔴 LIVE: WABUNGE WAKIMCHAPA MASWALI MAZITO WAZIRI MKUU BUNGENI

Nukta TV

CEO, TAB Group: Africa Agri Expo 2026 inakwenda kufungua fursa kimataifa, kilimo cha Tanzania

CEO, TAB Group: Africa Agri Expo 2026 inakwenda kufungua fursa kimataifa, kilimo cha Tanzania

Nukta TV

TANTRADE: Tumieni vifungashio vya "Made in Tanzania"

TANTRADE: Tumieni vifungashio vya "Made in Tanzania"

Nukta TV