Wasichana wang’ara matokeo darasa la nne, kidato cha pili

January 10, 2026 3:29 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Zaidi ya wanafunzi milioni 1.5 washiriki upimaji wa darasa la nne nchini
  • Ufaulu wa kidato cha pili waongezeka kwa asilimia 1.52 ndani ya miaka miwili.

Dar es Salaam. Wasichana wameendelea kung’ara katika matokeo ya upimaji wa kitaifa wa darasa la nne, kidato cha pili kwa mwaka 2025, kulingana na matokeo yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta).

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Said Mohamed aliyekuwa akizungumza leo Januari 10, 2026 jijin Dar es Salaam, amesema katika upimaji wa darasa la nne uliofanyika Oktoba 22 na 23, 2025 wasichana wamefaulu kwa asilimia 90.1 huku wavulana wakifaulu kwa asilimia 87.59.

“Jumla ya wasichana 703,287 wamefaulu, sawa na asilimia 90.1 ya wasichana wote waliofanya upimaji huo,” ameeleza Dk Mohamed.

Kwa mujibu wa matokeo hayo, ufaulu wa jumla kwa darasa la nne ni asilimia 88, ikiwa ni ongezeko la asilimia 2.67 ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Kwa mwaka 2025, wanafunzi 1,583,686 walisajiliwa kufanya mtihani wa upimaji wa darasa la nne wakiwemo wasichana 818,673 sawa na asilimia 52 na wavulana 765,013 sawa na asilimia 48.

Idadi yawabeba wasichana

Kwa upande wa wa upimaji wa kidato cha pili asilimia 56 ya wasichana wamefaulu wakiwapita wavulana waliofaulu kwa asilimia 44.

Ingawa wavulana wameonyesha ufaulu wa juu kwa asilimia katika kidato cha pili, wasichana wameng’ara katika matokeo hayo  kutokana na idadi yao kuwa kubwa.

Katika mtihani huo uliofanyika Novemba 10 hadi 19, 2025, jumla ya wanafunzi 898,718 walijiandikisha, wakiwemo wasichana 497,891 sawa na asilimia 55.48 na wavulana 400,827 sawa na asilimia 44.52. 

Aidha, ufaulu wa jumla wa kidato cha pili kwa mwaka 2025 ni asilimia 86.93, sawa na wanafunzi 705,091. 

Kati yao, wavulana 312,492 wamefaulu, sawa na asilimia 88.28 ya wavulana waliofanya mtihani, huku wasichana wakiwa 392,599 sawa na asilimia 85.89 ya wasichana wote walifanya mtihani.

Katika mtihani huo uliofanyika Novemba 10 hadi 19, 2025, jumla ya wanafunzi 898,718 walijiandikisha, wakiwemo wasichana 497,891 sawa na asilimia 55.48 na wavulana 400,827 sawa na asilimia 44.52. 

Dk Mohamed ameongeza kuwa ufaulu wa kidato cha pili umeendelea kuimarika, ukiongezeka kwa asilimia 1.52 kutoka asilimia 85.41 mwaka 2024 na asilimia 85.31 mwaka 2023.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...

Enable Notifications OK No thanks