Wanahabari, wanasayansi waandaliwa ruzuku kupambana na Corona Tanzania

June 3, 2020 10:09 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Wanatakiwa kufanya utafiti na kuja na suluhisho la changamoto ya maambuki ya Corona Afrika.
  • Ruzuku hiyo ya Sh10.9 bilioni itatumika katika nchini 17 za Afrika ikiwemo Tanzania. 
  • Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) kusimamia suala hilo Tanzania.

Dar es Salaam. Mapambano dhidi ya ugonjwa wa virusi vya Corona yanaendelea duniani kwa kutumia njia mbalimbali zikiwemo za kisayansi kutokomeza kabisa maradhi hayo yaliyoharibu uchumi wa dunia.  

Sasa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) imetangaza fursa kwa wadau wa utafiti, waandishi wa habari za sayansi na afya, mawasiliano pamoja na washauri wa masuala yakisayansi inayolenga kuibua suluhu dhidi ya COVID-19 ikiwemo kusaidia watu kupata taarifa sahihi juu ya ugonjwa huo.

Fursa hiyo ya Covid-19 Africa Grant Fund itatoa ruzuku ya Sh10.9 bilioni  katika nchi 17 za Afrika ikiwemo Tanzania ambapo wahusika wanatakiwa kuzitumia kuleta suluhisho la ugonjwa huo barani Africa.

Ruzuku hiyo imetolewa na Mfuko wa Taifa wa Utafiti wa Kusini mwa Afrika (NRF) kwa kushirikiana masharika ya kimataifa na tume za sayansi na teknolojia za nchi za Afrika.

Nchi zingine zinazoweza kushiriki ni pamoja na Botswana, Burkina Faso, Ivory Coast, Ethiopia, Ghana, Kenya na Malawi

Pia Msumbiji, Namibia, Rwanda, Senegal, Afrika Kusini, Uganda, Zambia, Zimbabwe na Nigeria.

Ruzuku hiyo imegawanyika katika maeneo matatu ya utafiti, mawasiliano na habari na masuala ya sayansi.

Kwa wadau wa utafiti, watahitajika kuibuka na tafiti zenye matokeo chanya juu ya COVID-19 zinazoweka wazi masuala ya kujikinga, Mfumo wa utawala wa kiafya wa nchi za Afrika, mwenendo wa maambukizi kijamii na kitamaduni, afya ya akili na mazingira yanavyochangia kuendelea kwa maambukizi.


Zinazohusiana


Kwa upande wa wadau wa mawasiliano ya kisayansi, taarifa ya Costech imesema wanatakiwa kuwa watu wanaotoa taarifa za kisayansi zinazosaidia wasomaji kupata chambuzi na taarifa sahihi na kupambana na habari zisizo za kweli.

Washauri wa masuala ya kisayansi, wanatakiwa kuwa watu wanaosaidia akademia za kiafrika na wanasayansi wachanga wakiafrika kwa ushauri kikanda na kibara juu ya muitikio wa Covid-19.

Hata hivyo, kwa upannde wa kipengele cha utafiti, ni nchi mbili tu ndiyo watu au taasisi zake zinaruhusiwa kushiriki ambazo ni Nigeria na Afrika Kusini.

Hiyo ni fursa kwa wanahabari na washauri wa masuala ya sayansi kufanya tafiti juu ya COVID-19 na kuja suluhisho litakalotumika barani humo.

Costech imeeleza kuwa mwisho wa kutuma maombi ni Juni 17, 2020 na zitapokelewa kupitia tovuti maalumu kwa lugha ya Kiingereza na Kifaransa. Maelekezo juu ya mfumo wa uandishi (Framework) yanapatikana hapa.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW