Wagonjwa wa afya akili waongezeka kwa asilimia 89, Serikali yaanika mikakati kuwakabili

May 11, 2026 4:29 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Wagonjwa wa afya ya akili 254,932 walihudumiwa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.
  • Changamoto hizo ni pamoja na sonona, utegemezi wa dawa za kulevya pamoja na matatizo mengine ya akili.

Dar es Salaam. Idadi ya wananchi waliopata huduma za afya ya akili na msaada wa kisaikolojia na kijamii nchini imeongezeka kwa asilimia 89.3  katika kipindi cha miaka miwili, huku Serikali ikianika mikakati mipya ya kukabiliana na changamoto hiyo.

Mohamed Mchengerwa, Waziri wa Wizara ya Afya aliyekuwa akiwasilisha bajeti yake kwa mwaka wa fedha 2026/2027 leo Mei 11, 2026 bungeni jijini Dodoma amesema Serikali mkakati hiyo imewekwa kwa makundi maalum yakiwemo watoto, wazee na watu wenye ulemavu. 

“Wateja 254,932 (wenye changamoto ya afya ya akili) walihudumiwa katika kipindi cha Julai 2025 hadi Machi 2026. Huduma hizo zilijumuisha matibabu ya kifafa, skizofrenia, matatizo ya tabia, pamoja na utegemezi wa pombe na dawa za kulevya,” amesema Waziri Mchengerwa.

Kwa mujibu wa takwimu hizo, idadi hiyo imeongezeka kwa asilimia 89.3 kutoka wagonjwa 134,643 waliopata huduma katika kipindi cha Julai 2024 hadi Machi 2025, sawa na ongezeko la wagonjwa 120,289.

Jenista Mhagama, aliyekuwa Waziri wa Afya wa wakati huo, alisema idadi hiyo ya wagonjwa wenye changamoto za afya ya akili ndani ya kipindi hicho waliongezeka kwa  asilimia 89.1 ikilinganishwa na wagonjwa wote 75,409 waliohudumiwa katika kipindi cha Julai 2024 hadi Machi 2025.

Afya ya akili  akili  ni miongoni mwa masuala yanayozikabili jamii nyingi nchini Tanzania na duniani kwa ujumla ikichangiwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ugumu wa maisha.

Mwaka 2025, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilibainisha kuwa zaidi ya watu milioni 300 wanahitaji huduma za afya ya akili na msaada wa kisaikolojia, jambo linaloonesha ongezeko kubwa la mahitaji haya muhimu. 

Kwa kutambua umuhimu wa suala hilo, Wizara ya Afya imeweka suala la afya ya akili kuwa miongoni mwa vipaumbele 11 vya wizara hiyo ambavyo vitatumia Sh1.8 trilioni katika mwaka wa fedha 2026/27 fungu 52. 

Kati ya fedha hizo, Sh1.148 trilioni ambazo ni sawa na asilimia 64 ya bajeti iliyotengwa zitatumika kutekeleza miradi ya maendeleo, fedha za ndani zikiwa ni Sh789.45 bilioni na kiasi cha Sh358.56 bilioni zinatoka kwa washirika wa maendeleo. 

Wagonjwa wa akili wahalifu waongezeka

Katika hatua nyingine, Waziri huyo ameeleza kuwepo kwa ongezeko la wagonjwa wa akili wahalifu waliothibitishwa na vyombo vya sheria na wanaopatiwa matibabu katika Hospitali ya Isanga.

Amesema hadi sasa jumla ya wagonjwa 474 waliothibitishwa kisheria wanaendelea na matibabu katika kituo hicho, jambo linaloonyesha hali kuongezeka kwa changamoto za afya ya akili zinazohusishwa na mazingira ya kijamii na kiuchumi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: WABUNGE WAKIWACHAPA MASWALI MAWAZIRI | Bunge la 13 | Mkutano wa 26

🔴LIVE: WABUNGE WAKIWACHAPA MASWALI MAWAZIRI | Bunge la 13 | Mkutano wa 26

Nukta TV

🔴LIVE: RAIS SAMIA AKIHITIMISHA MAFUNZO YA UONGOZI NGAZI YA JUU, UONGOZI DARAJA LA PILI KOZI 2025/26

🔴LIVE: RAIS SAMIA AKIHITIMISHA MAFUNZO YA UONGOZI NGAZI YA JUU, UONGOZI DARAJA LA PILI KOZI 2025/26

Nukta TV

Rais Samia: Anzisheni mfuko  kuwasaidia wafungwa wenye ujuzi wanapotoka gerezani

Rais Samia: Anzisheni mfuko kuwasaidia wafungwa wenye ujuzi wanapotoka gerezani

Nukta TV