Wafanyabiashara, wakulima waneemeka bei ya maharage ikipanda

January 24, 2020 2:49 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Bei ya juu ya maharage ya gunia la kilo 100 inauzwa Sh290,000 katika masoko ya Tandika na Kinondoni jijini Dar es Salaam ikiwa imepanda kutoka Sh280,000 iliyorekodiwa wiki iliyopita jijini humo na mkoani Mtwara. 
  • Bei ya chini zao hilo imeshuka hadi  Sh120,000 kwa gunia moja katika mkoa wa Kagera ikilinganishwa na Sh140,000 iliyokuwepo wiki iliyopita katika mkoa wa Arusha. 

Dar es Salaam. Wafanyabiashara na wakulima wa maharage katika baadhi ya maeneo nchini Tanzania watamaliza wiki na tabasamu baada ya bei ya zao hilo kupanda ikilinganishwa na wiki iliyoishia Januari 17, 2020.

Kwa mujibu wa takwimu za bei za jumla za mazao makuu ya chakula nchini zilizotolewa leo Januari 24, 2020 na Wizara ya Viwanda na Biashara, zinaonyesha kuwa bei ya juu ya maharage ya gunia la kilo 100 inauzwa Sh290,000 katika masoko ya Tandika na Kinondoni jijini Dar es Salaam ikiwa imepanda kutoka Sh280,000 iliyorekodiwa wiki iliyopita jijini humo na mkoani Mtwara. 

Hiyo ina maana kuwa kwa kila gunia moja, mfanyabiashara atapa Sh10,000. 

Hata hivyo, bei ya chini zao hilo imeshuka hadi  Sh120,000 kwa gunia moja katika mkoa wa Kagera ikilinganishwa na Sh140,000 iliyokuwepo wiki iliyopita katika mkoa wa Arusha. 

Ifahamike kuwa utaratibu wa kutoa bei za jumla za mazao makuu ya chakula hufanyika mara tatu kwa wiki yaani Jumatatu, Jumatano na Ijumaa. 

Bei za juu za mchele zimebaki kama zilivyorekodiwa wiki iliyopita za Sh150,000 katika mkoa wa Kigoma huku bei ya chini ikishuka kutoka Sh280,000 jijini Dar es Salaam hadi Sh270,000. 

Pia bei ya juu ya mahindi  imepanda kutoka Sh78,000 iliyorekodiwa mkoani Rukwa hadi Sh80,000 iliyorekodiwa leo mkoani Ruvuma. Lakini bei ya chini imeshuka kutoka Sh120,000 kama ilivyorekodiwa mkoani Mwanza hadi Sh110,000 katika jijini Dar es Salaam na Tabora na kuwapa ahueni wananchi wa mikoa hiyo.  

Enable Notifications OK No thanks