Viwango vya kubadilisha fedha Tanzania Januari 7, 2026
Hivi ndivyo viwango vya kubadilisha fedha za kigeni dhidi ya Shilingi ya Tanzania vilivyotolewa na Benki zaCRDB na NMB kwa matumizi ya leo Januari 7, 2026.
viwango hivi hubadilika kila siku kulingana na mwenendo wa soko la fedha, na vina umuhimu mkubwa kwa wafanyabiashara, wawekezaji na walipakodi, hasa katika kufanya malipo ya ada, kodi pamoja na ununuzi na uingizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi.
Kupitia viwango hivi vya kubadilisha fedha, watumiaji wa sarafu za kigeni hupata mwongozo sahihi wa kupanga bajeti, kufanya manunuzi na kuendesha shughuli zao za kifedha kwa ufanisi zaidi
Kwa siku ya leo Dola ya Marekani kupitia Benki ya CRDB imeuzwa kwa bei ya reja reja ya Sh2,440 na kunuuliwa kwa Sh2,520.
Bei hiyo inayotumika leo imeongezeka kwa Sh10 kutoka bei ya kuuza na kunua Dola hiyo ya Marekani iliyotumika Januari Mosi mwaka huu.
Kwa upande wa NMB thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani imeongezeka kwa Sh10 kutoka bei ya kuuza na kunua Dola hiyo ya Marekani iliyotumika Januari Mosi mwaka huu.
Hata hivyo, fedha nyingine kutoka mataifa mengine duniani zimeendelea kuimarika au kushuka kama inavyoonekana ikiashiria mabadiliko ya nguvu ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya sarafu za kimataifa.

Latest