Vipi, tukuletee Konyagi ama Chibuku?

January 23, 2020 12:45 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Dar es Salaam. Ukiachana na bia, vilevi vingine vinavyozalishwa kwa wingi viwandani #Tanzania ni Konyagi na Chibuku. Takwimu rasmi zinaonyesha bia lita 412.6 milioni zilizalishwa mwaka 2018 zikifuatiwa na Konyagi.

Uzalishaji wa bia mwaka huo, kwa mujibu wa Kitabu cha Hali ya Uchumi wa Taifa mwaka 2018, ulikuwa ni mara nane zaidi ya lit azote za Konyagi na Chibuku. Chibuku ni moja vilevi vya kiwandani vyenye bei nafuu nchini wakati Konyagi ikisifika kwa kuwa kilevi imara zaidi.

Ukiachana na bia, ambazo zinatengenezwa na kampuni mbalimbali, iwapo utaangalia takwimu hizo kwa kina mwenendo katika baadhi ya miaka mitano iliyopita, Konyagi na Chibuku ni kama zilikuwa zinachuana katika kiwango cha uzalishaji.

Ikumbukwe kuwa vinywaji vyote hivyo viwili vinatoka katika familia moja ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
16 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Nukta TV

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Nukta TV

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV