Uzushi: Watu waliopata chanjo ya Corona hawatakufa baada ya miaka miwili

July 13, 2021 2:50 pm · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Amezushiwa kuwa amesema chanjo ina madhara na waliopata watakufa baada ya miaka miwili.
  • Wametumia mahojiano yake aliyofanya na kipindi cha televisheni cha France 24.
  • Montagnier amekanusha kuwa alinukuliwa vibaya.

Dar es Salaam. Baada ya mtaalamu wa afya Luc Montagnier kufanya mahojiano katika kipindi cha ‘Hold up’ kinachohusu masuala ya COVID-19 nchini Ufaransa, watu wamemnukuu vibaya na kusambaza habari za uzushi kwenye mitandao ya kijamii hasa Whatsapp.

Wamemzushia kuwa amesema watu wote waliopata chanjo ya Corona watafariki baada ya miaka miwili.

Habari hiyo iliyopo kwenye mfumo wa video katika mitandao mbalimbali ikiwemo Twitter, inamhusisha mtangazaji na Montagnier ambaye ni mshindi wa tuzo ya Nobel mwaka 2008 wakiongea kwa lugha ya kifaransa kuhusu matokeo ya chanjo za Corona zilizoanza kufanya kazi mwanzoni mwa mwaka huu.

Hata hivyo, habari hiyo haina ukweli wowote kwasababu katika mahojiano hayo Montagnier aliongelea madhara ya chanjo ya Corona, lakini hakusema watu watakaopokea chanjo hiyo watakufa baada ya miaka miwili.

Baada ya video hio kusambaa mtandaoni, Montagnier aliandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter ukisema, “Were the claims misinterpreted? Does it really mean that vaccination will cause death or its consequences would make complications?”

Ujumbe huo unamaanisha kuwa “Madai yalieleweka vibaya? Yalimaanisha chanjo zitasababisha vifo au matokeo yataleta shida?”

Pamoja na kwamba Montagnier aliongelea madhara ya chanjo ya ugonjwa wa Corona, lakini hakusema mtu anapopata chanjo hiyo atakufa baada ya miaka miwili.

Uzushi: Mshindi wa tuzo ya Nobel Montagnier hajasema watu waliopata chanjo ya Corona watakufa baada ya miaka miwili

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV