Uzushi: Rais Macron wa Ufaransa hajashambuliwa kwa kukiuka tahadhari ya Corona

July 9, 2021 11:40 am · Daniel
Share
Tweet
Copy Link
  • Wapotoshaji wamesambaza picha inayoonyesha Rais Macron akiwa na alama za vidole usoni baada ya kupigwa kibao.
  • Picha hiyo inasema amepigwa kwa sababu hajachukua tahadhari ya Corona.
  • Habari picha hiyo haina ukweli wowote bali ni uzushi.

Dar es Salaam. Kuna picha inayosamba kwenye makundi ya Whatsapp na mitandao mengine ya kijamii kama Facebook  inayodai kuwa Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron amepigwa kofi baada ya kukikuka masharti ya Corona (COVID-19), siyo ya kweli.

Habari picha hiyo inapotosha kwa sababu hakuna tukio kama hilo kwa Rais Macron.

Picha hiyo iliyoambatana na maneno katika lugha ya Kiingereza inasema “France courts have delivered judgement on the case of President Macron being slapped by a man on the side stands.The  learned counsel of the victim says the president disobeyed COVID-19 Protocols by doing handshakes & Not observing the 1.5m Rule hence the accused reacted to anger & decided to teach their President a lesson. The accused is set to be free”

Katika tasfri isiyo rasmi inasema “Mahakama nchini Ufaransa imetoa hukumu kwa mtu aliyempiga kofi Rais Macron. Wakili wa mshtakiwa amesema Rais alidharau masharti ya Corona (COVID-19) kwa kushikana mikono na kutozingatia masharti ya mita moja na nusu hali hiyo ilishababisha mshtakiwa kupatwa na hasira na kuamua kumfundisha adabu Rais. Mshtakiwa ameachiwa huru,”

Ukweli uko wapi

Ni kweli Macron alikumbana na kadhia hiyo Juni 8 mwaka huu alipotembelea  chuo cha mafunzo stadi  ya utalii   usimamizi wa hoteli huko Tain-l’Hermitage.

Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Damien Trel alimpiga Macron kofi kwa mkono wake mmoja wakati alipokuwa amemshika kwa mkono wake mwingine.

Hata hivyo, tukio hilo halina uhusiano wowote na COVID-19.

Kwa kutumia zana ya kijigitali ya ‘Reverse Image Search’ inaonyesha picha iliyotumika kupotosha ilichapishwa mtandaoni kwa mara ya kwanza Mei 26, 2021, ikiwa ni siku chache kabla ya Rais Macrom kushambuliwa.

Picha hiyo haionyeshi kama amevaa barakoa wala alama yoyote ya vidole vilivyobaki katika uso wake.

Vilevile  mshtakiwa Trel aliyempiga Rais Macrom kibao hajaachiwa huru tofauti na maelezo ya picha hiyo. Amehukumiwa kifungo cha miezi minne.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW