Unavyoweza kuwa mtoa huduma bora kwa mteja wako

October 2, 2021 8:42 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pamoja na kutoa ushauri wa bure kwa mteja wako.
  • Pia kutumia lugha chanya badala ya lugha hasi.
  • Toa huduma na bidhaa bora zinazokidhi mahitaji yake.

Dar es Salaam. Wafanyabiashara wengine wanaweza kuishia kukuharibia siku yako hata kama uliamka na siku yako ilionekana kuwa njema kabisa. 

Siku moja nilikuwa na dada yangu na aliamua kununua parachichi gengeni. Kwa kuwa alijua namie tumbo langu litadai, alihitaji parachichi kubwa kidogo ili tutoshee wote.

“Naomba parachihi kubwa la 1,000,” dada yangu alimwambia muuza genge. Na muuza alichukua parachichi na kumpa. 

Pale dada yangu alipouliza kama anaweza kupata la 1,000 ambalo ni kubwa kidogo kuliko alilopewa, jibu la muuzaji lilikuwa, “umetaka parachichi la buku na hilo ndio la buku,” kwa maandishi inaweza kusomeka kama jibu zuri tu lakini sauti yake, haikuwa ya kistaarabu wala ya kumkarimu mteja.

Tuliondoka na dada yangu na licha ya kuwa anaendelea kununua matunda pale sokoni, hajawahi kununua tena kitu kwa muuza genge yule.

Inaonyesha ni kiasi gani huduma yako ya mara ya kwanza inaweza kuendelea kukuletea wateja kila siku au siku ya kwanza ya mteja wako ndiyo ikawa ya mwisho. 

Unawezaje kuwatunza watu watakaoruka maduka au magenge ambayo wanayaona njiani na kuja kwako moja kwa moja? 

Ni pamoja na kumsikiliza mteja anachokitaka, kutumia lugha chanya na kumshauri mteja ili apate kitu bora zaidi.

Zaidi, jifunze kupitia video hii fupi.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
6 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
6 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Fahamu kuhusu 'BIPOLAR' | Ugonjwa hatari unaoathiri na kubadili hisia

Fahamu kuhusu 'BIPOLAR' | Ugonjwa hatari unaoathiri na kubadili hisia

Nukta TV

Je, ’BIPOLAR’ ina uhusiano na kupenda kufanya tendo la ndoa zaidi?

Je, ’BIPOLAR’ ina uhusiano na kupenda kufanya tendo la ndoa zaidi?

Nukta TV

Hii ndio sababu uhusiano wa kimapenzi ni marufuku makazini

Hii ndio sababu uhusiano wa kimapenzi ni marufuku makazini

Nukta TV