Unavyoweza kuepuka ugonjwa wa kiharusi

September 27, 2021 4:17 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ugonjwa huo hugharimu maisha ya watu milioni tano kila mwaka.
  • Wanaopoteza maisha zaidi ni wanaume kuliko wanawake.
  • Mtindo mzuri wa maisha unaweza kupunguza hatari ya kupata kiharusi.

Dar es Salaam. Ugonjwa wa kiharusi ni miongoni mwa magonjwa yanayowatesa zaidi watu duniani kutokana na kuhusishwa na mtindo wa maisha ikiwemo uzito uliopitiliza. 

Ugonjwa huo hutokea pale kiwango cha damu inayohitajika kwenye ubongo kinapoingiliwa au kupungua na kusababisha uhaba wa hewa ya oksijeni au virutubishi kufikia ubongo.

Pia, kiharusi kinaweza kusababishwa na damu kuvujia kwenye ubongo.

Hali hiyo inaweza kusababishwa na kurundikana kwa mafuta kwenye mishipa ya ubongo na hivyo kuzuia damu kusafiri inavyotakiwa.

Kwa mujibu wa kituo cha utafiti wa masuala ya afya cha Mayo Clinic, cha  Marekani, dalili za ugonjwa huo ni pamoja na ganzi kwenye uso, miguuni au mikononi, kupata changamoto ya kuelewa kinachozungumzwa na mtu, changamoto ya kuona kwa macho yote, kichwa kuuma na shida ya kutembea.

Kiharusi kinavyosumbua dunia

Licha ya kuwa ugonjwa huo ni maarufu miongoni mwa watu wenye umri mkubwa, bado umechukua nafasi kwenye maisha ya watu wenye umri mdogo.

Takwimu za mwaka 2019 kutoka kwa Shirika la Ugonjwa wa Kiharusi Duniani (WSO), zinaeleza kuwa, ugonjwa huo huwakumba watu milioni 13.7 kila mwaka.

Kati ya watu hao, asilimia 60 ni wale wenye umri wa miaka 45 hadi 70 huku asilimia 8 ikiwa ni ya watu wenye umri chini ya miaka 44.

Zaidi ni kuwa, kwa mwaka watu milioni 5.5 hupoteza maisha duniani kutokana na ugonjwa huo wengi wakiwa ni wanaume kwa asiimia 53.

                     

Vichochezi vya ugonjwa wa kiharusi

Tovuti ya masuala ya afya ya Web MD imeeleza kuwa  ugonjwa huo unaweza kuchochewa na magonjwa mengine ikiwemo presha lakini mtindo wamaisha wa mtu pia unaweza kumchochea kupata kiharusi.

Matahalan, matumizi ya tumbaku na bidhaa zake, kuwa na uzito uliopitiliza pamoja na umri.

Web MD imeandika, “mtu yeyote anaweza kupata kiharusi, hata watoto wakiwa tumboni. Uwezekano wa mtu kupata ugonjwa huo huenda juu kadili sumri unapoongezeka. Uwezekanohuongezeka mara mbili kwa kila muongo mt akishafikisha miaka 5.” 

Ili kuepukana na ugonjwa huu,  Mayo Clinic inashauri kuhakikisha usawa kwenye presha ya damu, kupunguza ulaji wa vyakula venye mafuta mengi (bad cholestrol), kuhakikisha mwili unauzito wa wastani na kula chakula chenye lishe kamili.

Tazama video hii kujifunza zaidi

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV