Unaandaa sherehe ya harusi wakati wa corona? Zingatia haya

July 24, 2020 4:03 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Pendelea kutumia ukumbi wa nje ikiwa ni pamoja na bustani au sehemu yenye mzunguko mzuri wa hewa.
  • Hakikisha vitu muhimu vya usafi kama maji tiririka, sabuni na tishu havikosekani katika eneo lako la sherehe.
  • Wakumbushe wageni wako kuzingatia protokali za kuzuia maambukizi pale wamapokuwa wanapiga chafya au kukohoa.

Dar es Salaam. Miongoni mwa mikusanyiko ambayo ilishauriwa kutokuwepo miezi kadhaa iliyopita ili kujikinga na janga la Corona ilikuwa ni sherehe za harusi. 

Hata hivyo, mnamo Juni 16, 2020 wakati Rais John Magufuli akitoa hotuba ya kulivunja bunge la 11, alisema shuguli zote zikiwemo shughuli za harusi zinaweza kuendelea huku akishauri Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona.

Unawezaje kuchukua tahadhari wakati wa kuandaa sherehe za harusi?

1. Chagua ukumbi wa nje au ulio na mfumo mzuri wa kupitisha hewa

Shirika la Afya Duniani (WHO) limependekeza pale unapochagua ukumbi, pendelea kuchagua ukumbi ambao upo nje kwa maana ya bustani au sehemu maalumu lakini isiwe ndani.

Endapo utalazimika kutumia ukumbi wa ndani, WHO inashauri uchague ukumbi ambao una mfumo mzuri wa kubadilisha hewa (ventilation system)

Pendelea kuchagua ukumbi ambao upo nje kwa maana ya bustani au sehemu maalumu lakini isiwe ndani. Picha| Willowsevents.

2. Hakikisha wageni wanakaa umbali unaohitajika

Wakati wa sherehe, hakikisha hakuna mikusanyiko baina ya wageni waalikwa, hilo linawezekana kwa kuwashauri waendelee kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya corona zikiwemo za kuzingatia umbali wa mita moja baina ya mtu na mtu.

3. Hakikisha kuna vifaa vya usafi

Una wajibu wa kuhakikisha usalama wa wageni wako wakati wa sherehe. Hivyo wakati wa maandalizi yako ni vyema ukachagua sehemu ambayo kuna vifaa vya usafi ikiwemo maji tiririka na sabuni.

Unashauriwa pia kuhakikisha tishu, vyombo vya kutupia taka na vitakasa mikono vinatosheleza sherehe yako.


Zinazohusiana


Pia, unashauriwa kuwasiliana na wageni waalikwa ili endapo yupo ambaye hajisikii vizuri ashauriwe kubaki nyumbani.

Pangilia vizuri ukumbi wako kuhakikisha wageni wanakaa kwa umbali unaopendekezwa. 

Kampuni ya The Knot inayojishughulisha kuandaa sherehe nchini Marekani wameshauri pia kupunguza idadi ya wageni wanaohudhuria harusi ili kuepuka msongamano. 

Ili kuhakikisha sherehe inafanikiwa waalikwa ambao hawajafika ukumbini wanaweza kufuatilia shughuli zote kwa njia ya mtandao ikiwemo kutumia mawasiliano ya video kama Zoom au Google Meet. 

Enable Notifications OK No thanks