Ufaransa yatoa Sh592 bilioni kuboresha huduma za maji, umeme Tanzania

June 30, 2020 8:41 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Doto James na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavier wakisaini moja ya Mikataba ya Mkopo nafuu wa 592.57 bilioni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya nishati na maji nchini. Anayeshuhudia katikati ni Mwakilishi mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (ADF) Stephanie Essombe, Jijini Dar es Salaam jana. Picha| Wizara ya Fedha na mipango.


  •  Mkopo huo utasaidia kutekeleza miradi mitatu ikiwemo ya maji katika mji wa Morogoro na usambazaji wa umeme vijijini katika mikoa 16.  
  • Serikali yasema miradi hiyo itaongeza kasi ya maendeleo kwa wananchi wa maeneo husika. 

Dar es Salaam. Wakazi wa miji inayozungumza Ziwa Victoria nchini Tanzania watakuwa ni miongoni mwa wanufaika wa mikopo yenye masharti nafuu kutoka Ufaransa inayokusudia kuboresha huduma za jamii ikiwemo maji na umeme. 

Serikali ya Tanzania na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) zimetiliana saini mikataba mitatu ya mikopo yenye masharti nafuu ya Sh592 bilioni kwa ajili ya miradi ya usambazaji wa maji na umeme vijijini.

Katika mradi wa usambazaji wa umeme vijijini utagharimu Euro milioni 100 (Tsh. bilioni 257.64) na utasambazwa katika mikoa 16 ya Tanzania Bara na Mradi wa Umeme wa Kuunganisha Tanzania na Zambia. 

Mikataba ya mikopo hiyo imesainiwa Juni 29, 2020 Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James, Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier na Mkurugenzi Mkazi wa AFD Stephanie Mouen Essombe.

Mradi wa usambazaji wa umeme vijijini utagharimu Euro 100 milioni  (Sh257.64 bilioni)  utatekelezwa katika mikoa 16 ya Tanzania Bara na mradi wa umeme wa kuunganisha Tanzania na Zambia.

Kwa upande wa mradi wa maji utawezesha upatikanaji wa maji Mji wa Morogoro kutoka mita za ujazo 33,000 hadi kufikia mita za ujazo 108,000 kwa siku. 

Hiyo itasaidia kufikia kiwango cha mahitaji ya maji safi kinachokadiriwa kuwa mita za ujazo 126,253 kwa siku ifikapo mwaka 2035. 

James katika taarifa yake iliyotolewa na Wizara ya Fedha na Mipango amesema miradi yote mitatu ambayo imesainiwa inawiana na Dira ya Maendeleo ya Tanzania ya mwaka 2025, ambayo kwa sasa inatekelezwa kupitia awamu ya pili ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (FYDP II) 2016/17 – 2020/21. 

Tanzania imekuwa ikinufaika na ufadhili wa AFD hususan katika sekta za nishati, maji, usafirishaji na kilimo kupitia miradi  mbalimbali inayoendelea na ile inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.


Zinazohuziana:


Mikopo hiyo utachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya nchi na kupunguza umaskini hasa kwa wananchi wanaokabiliwa na changamoto za upatikanaji wa maji na umeme.

“Ushirikiano wa Tanzania na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) ulioanza miaka 20 iliyopita umezidi kuimarika ambapo katika kipindi cha miaka 10 iliyopita Shirika limewekeza kiasi cha Euro milioni 258 sawa na takriban Sh655 bilioni za Tanzania,” amesema Stephanie Mouen Essombe, Mkurugenzi Mkazi wa AFD.  

Amesema mradi wa maji  katika mji wa Morogoro   unalenga kupanua bwawa la Mindu linalochangia upatikanaji wa maji yanayotumika katika mji huo kwa asilimia 70 pamoja na kuboresha mfumo wa huduma ya maji taka katika mji huo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof Kitila Mkumbo amesema kuwa mkopo huo utatatua changamoto ya maji ambayo ilikuwa kilio cha muda mrefu kwa wananchi wa Morogoro.

Mkopo huu una faida nyingi ikiwemo kutoa na fursa kwa viwanda vya ndani kwa sababu vifaa vitakavyotumika kutekeleza mradi huo wa kihistoria vitanunuliwa Tanzania. 

Amesema upatikanaji wa fedha hizo ambazo mjadala wa kupata mkopo umechukua zaidi ya miaka minne utawezesha kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji nchini ambapo hivi sasa kiwango cha upatikanaji wa maji vijijini kimefikia asilimia 85 ya lengo la asilimia 95.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW