Twitter kuwawekea watumiaji wake kipengele cha kupanga picha kwa mtiririko wanaoutaka

August 1, 2019 6:12 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Kipengele hicho kiko kwenye majaribio na kikamilika kitawapa uhuru zaidi watumiaji wa mtandao huo.
  • Itakuwa ahabari njema kwa watu wanaopenda kupanga picha kwa mtiririko wanaoutaka katika mabandiko yao.  

Hatimaye changamoto wanayoipata watumiaji wa mtandao wa Twitter ya kupanga picha watakavyo katika mabandiko (post) Yao itafika mwisho, baada ya suluhisho kupatikana. 

Kwa mujibu wa ugunduzi uliofanywa na Mtaalam wa kujitegemea wa masuala ya mitandao ya kijamii, Jane Manchun Wong, Twitter inafanyia kazi kipengele kipya ambacho kitamuwezesha mtu kupanga picha kwa mtiririko anaoutaka kwa kutumia mchakato rahisi wa  ‘drag and drop’. 

Huenda hiyo itakua habari njema kwa watumiaji wa mtandao huo, ikizingatiwa kwa sasa hawezi kupanga picha katika mtiririko wanaoutaka  wakati wanaweka ujumbe Twitter. 

Mabadiliko hayo ni madogo lakini yana maana kubwa kwa watumiaji ambao wanapenda kuwa na machaguo mbalimbali wakati wakitumia mtandao huo. Pia itaondoa usumbufu wa kufuta na kuweka picha ili zikae kama mfumo wa Twitter unavyotaka. 

Hata hivyo, Twitter bado hawajazungumza neno lolote kuhusu mabadiliko hayo, lakini yatakapokamilika na kuanza kutumika yatakua ni habari njema kwa watumiaji wa mtandao huo unaokua kwa kasi duniani. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
26 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Elimu ya kodi mwarobaini wa wafanyabiashara kuikwepa TRA, ianzie shuleni

Elimu ya kodi mwarobaini wa wafanyabiashara kuikwepa TRA, ianzie shuleni

Nukta TV

Rais Samia: Serikali chini ya Magufuli haikutaka kuyumbishwa kukamili kwa JNHPP

Rais Samia: Serikali chini ya Magufuli haikutaka kuyumbishwa kukamili kwa JNHPP

Nukta TV

Rais Samia: Umeme wa SGR hautoingiliwa, Dodoma umeme uhakika 24/7

Rais Samia: Umeme wa SGR hautoingiliwa, Dodoma umeme uhakika 24/7

Nukta TV