Tume ya Chande yapokea simu za matusi 300 baada ya ripoti

April 28, 2026 4:21 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Yasema jumbe za matusi zinaashiria kuibuka kwa mwenendo hatari unaotishia misingi ya majadiliano ya kidemokrasia.
  • Yadai kuna kundi halitaki maoni yaliyowasilishwa na tume hiyo.

Dar es Salaam. Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 imesema tangu iwasilishe ripoti ya matukio hayo Aprili 23 mwaka huu imepokea simu za matusi zaidi ya 300.

Mjumbe wa tume hiyo na Jaji Mkuu mstaafu, Ibrahim Juma aliyekuwa akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo Aprili 28, 2026 simu hizo zimetokana na baadhi ya Watanzania kupinga maoni ya tume hiyo yaliwasilishwa hivi karibuni.

“Baada ya taarifa kutoka, tumepokea matusi zaidi ya 300 kwa sababu kuna mtu hataki maoni yetu yaliyopatikana kwa njia ya methodolojia ambayo sisi tumeyaorodhesha yasijulikane kwa watanzania ,” amesema.,” amesema Profesa Juma.

Hii ni  mara ya kwanza kwa tume hiyo kuzungumza na wanahabari baada ya kuwasilisha ripoti ya uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani iliyofanyika kwa siku 153 ukianisha hoja mbalimbali zilizoibua mijadala mipana katika jamii.

Profesa Juma amefafanua kuwa kupokea simu za matusi kunaashiria kuibuka kwa mwenendo hatari unaotishia misingi ya majadiliano ya kidemokrasia, ambapo baadhi ya watu wanajaribu kuzima maoni ya wengine badala ya kuyajadili kwa hoja. 

“Unaposema wewe ni muumini wa demokrasia na haki za binadamu kuwa tayari kusikiliza maoni na mawazo ambayo wewe hupendi kuyasikiliza,” amefafanua Prof Juma.

Ameongeza kuwa ni muhimu kuwa na soko la mawazo kutoka kwa watu tofauti na kushindana na sio kundi moja kutaka mawazo yake kusikika huku likishambulia mawazo ya kundi lingine kama nyuki.

Amefafanua kuwa ripoti ya tume hiyo iliandaliwa kwa kufuata misingi ya kitaalamu na mbinu shirikishi , ikiwemo kukusanya maoni ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali ili kupata taswira halisi ya matukio yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu uliopita. Hivyo, juhudi hizo zinapaswa kuheshimiwa badala ya kubezwa au kushambuliwa.

Pamoja na hayo, amebainisha kuwa tume imefanikiwa kukusanya ushahidi muhimu unaobainisha wahusika wa matukio hayo, wakiwemo waliopanga, kuratibu na kufadhili vitendo vya uvunjifu wa amani. 

Hata hivyo, amesisitiza kuwa tume haitakimbilia hatua za kuwawajibisha watu bila kuwapa nafasi ya kusikilizwa, kwa kuzingatia kanuni za haki asilia.

“Tumepata ushahidi wa waliopanga, walioratibu na waliohusika, lakini kwa misingi ya haki ni lazima wapewe nafasi kupitia utaratibu mwingine kujibu hoja na ushahidi wetu kabla ya hatua zozote kuchukuliwa,” ameeleza.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Mohamed Chande amesema tume itaendelea kusimamia ukweli na uwazi katika kazi zake, huku ikisisitiza kuwa maoni yaliyokusanywa ni sauti halali za wananchi na yanapaswa kupewa nafasi ya kusikilizwa bila vitisho wala kejeli.

Katika mkutano huo uliowahusisha wahariri na waandishi wa habari, Profesa Juma pamoja na wajumbe wengine walifafanua vipengele mbalimbali vilivyomo kwenye ripoti hiyo, wakisisitiza umuhimu wa kuijadili kwa kina ili kusaidia kuboresha mifumo ya uchaguzi na kudumisha amani nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
BALOZI JAMES: Hakuna mtanzania aliyeshambuliwa Afrika Kusini

BALOZI JAMES: Hakuna mtanzania aliyeshambuliwa Afrika Kusini

Nukta TV

🔴LIVE: TUME YA UCHUNGUZI MATUKIO OKTOBA 29, USO KWA USO NA WAANDISHI WA HABARI

🔴LIVE: TUME YA UCHUNGUZI MATUKIO OKTOBA 29, USO KWA USO NA WAANDISHI WA HABARI

Nukta TV

🔴LIVE: HOTUBA YA BAJETI WIZARA YA KILIMO IKIWASILISHWA BUNGENI

🔴LIVE: HOTUBA YA BAJETI WIZARA YA KILIMO IKIWASILISHWA BUNGENI

Nukta TV