TRA yavunja rekodi makusanyo ya kodi

January 2, 2023 10:52 am · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Yafikia asilimia 99 ya lengo la kukusanya Sh12.48 trilioni mwaka 2022/23.
  • Disemba yavunja rekodi ya kukusanya mapato mengi zaidi tangu kuanzishwa kwa TRA mwaka 1996.

Dar es salaam. Nusu ya mwaka wa fedha wa 2022/23 inaisha vizuri kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), mara baada ya kufanikiwa kukusanya kiasi cha Sh12.46 trilioni sawa na asilimia 99 ya lengo la makusanyo.

Katika nusu ya kwanza ya mwaka 2022/23, mamlaka hiyo ilijiwekea lengo la kukusanya Sh12.48 trilioni.

Makusanyo hayo ya fedha huenda yakarahisisha  upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii kama elimu, afya na maji ambazo hutegemea fedha kutoka Serikalini.

Kamishna Mkuu wa TRA Alphayo Kidata  katika taarifa yake iliyotolewa Januari Mosi mwaka huu ameeleza kuwa kiasi kilichokusanywa ni ongezeko la Sh1.35 trilioni ikilinganishwa na kiwango kilichokusanywa kwa kipindi kama hicho mwaka wa fedha 2021/22.

“Ongezeko hili ni sawa na ukuaji wa makusanyo wa asilimia 12.2,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.


Zinazohusiana:


Kwa mujibu wa TRA, mwezi Disemba imekusanya  Sh2.77 trilioni kati ya lengo la kukusanya Sh2.60  sawa na ukuaji wa asilimia 10.3 ukilinganisha na makusanyo ya mwezi Desemba 2021.

“Pamoja na makusanyo haya kuvuka lengo la mwezi Desemba 2022, ndicho kiwango cha juu zaidi kukusanywa kwa mwezi tangu kuanzishwa kwa mamlaka mwaka 1996, “ amesema Kidata katika taarifa hiyo.

Makusanyo haya ya nusu ya mwaka wa fedha 2022/23 ni sawa na nusu ya mapato ya kodi na yasiyo ya kikodi yaliyopangwa kukusanywa na TRA katika bajeti ya fedha ya mwaka 2022/23.

Mfumo wa bajeti wa mwaka 2022/23 uliotolewa na Wizara ya  Fedha na Mipango  unaonesha kuwa TRA inapaswa kukusanya Sh23.65 trilioni.

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV