Tofauti iliyopo tembo wa Afrika, Asia
- Ni pamoja na tofauti za maumbile
- Ukubwa wa masiko, pembe na muundo wa kichwa.
- Kwa muonekano pia, tembo wa Afrika ni mkubwa kuliko wa Asia.
Dar es Salaam. Huenda unadhani tembo ni tembo tu. Awe Ulaya, awe Marekani au kokote, ilimradi ni mkubwa na ana masikio makubwa na mkonga, basi ni mnyama yule yule.
Kama hiyo ni nadharia yako, ni muda wa wewe kuachana nayo kwani mnyama huyo naye ana aina zake na wanatofautiana kwa sifa mbalimbali ikiwemo kimuonekana kulingana mazingira waliyopo.
Makala haya yatakupatia tofauti ya tembo anayepatikana katika barala la Afrika na yule kutoka Bara la Asia.
Tembo wa Afrika ana masikio makubwa kuliko tembo wa Asia. Picha| safarisafricana.
Tofauti za maumbile
Kuna tofauti takriban 10 za kimaumbele ambazo zinaweza kukusaidia kutofautisha tembo wa Afrika na Asia.
Shirika la Uhifadhi Wanyama Pori (WWF) limebainisha kuwa, tembo wa bara la Asia ana masikio madogo ikilinganishwa na tembo wa Afrika.
Tofauti nyingine ni meno au pembe. Kwa tembo wa Asia, ni tembo dumbe ndiyo huota meno, tena siyo tembo wote na meno yao huwa madogo ikilinganishwa na tembo wa Afrika.
Kwa tembo wa Afrika, wote dume na jike huota pembe na pembe zao ni kubwa.
Hata tembo wa Afrika, nao wana aina mbili. WWF inaeleza kuwa, yupo tembo wa Savanna na wa msituni lakini hiyo ni mada ya siku nyingine.
Soma zaidi
- Kasa: Mnyama mpole mwenye maajabu mengi
- Ubabe wa kiboko mwisho mtoni
- Mambo yatakayosaidia uhifadhi endelevu wa wanyamapori Tanzania
Umbo la kichwa
Jambo lingine linalotofautisha tembo hawa ni maumbile ya vichwa vyao. Tovuti ya masuala ya utalii ya SafarisAfricana imeandika kuwa, vichwa vya tembo hao vinatofautiana kwa ukubwa na umbile la juu.
Tembo wa bara la afrika ana kichwa kikubwa na kina umbo la duara kwa juu. Tembo wa Asia vichwa vyao ni vidogo na vina kama nundu mbili.
Umbo la tembo wa Afrika ni kubwa pia na hata uzito wake ni mkubwa akilinganishwa na tembo wa Asia.
Tovuti ya ThomsonSafarisย inaeleza kuwa, ukubwa wa tembo wa Africa hunedna unasababishwa na uwezo wa mkonga wake kukamata chakula kingi na kupeleka mdomoni ikilinganishwa na tembo wa Asia.
Bila shaka sasa unaweza kuona tembo na ukajua kuwa huyo ni wa Afrika au ni wa Asia.
Latest
