Tanzania yazindua ujenzi wa bandari ya uvuvi ya Sh266 bilioni

September 19, 2023 2:01 pm · Husna Hassan
Share
Tweet
Copy Link
  • Wavuvi zaidi ya 100 kupata boti za kisasa.
  • Bilioni 266 kuwekezwa.

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezindua ujenzi wa bandari ya kwanza ya uvuvi nchini inayotarajiwa kuchochea uchumi wa wakazi wa mikoa ya kusini  ya Lindi na Mtwara.

Kukamilika kwa mradi huo utakaogharimu Sh266 bilioni, kutaisaidia Tanzania kukuza sekta ya uvuvi katika kuchangia katika pato la taifa na kutengeneza ajira kupitia uchumi wa bluu.

Ujenzi wa bandari hiyo iliyopo Kilwa Masoko mkoani Lindi ulianza tangu Februari 2022 na unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 24. Mara baada ya kukamilika itafanyiwa majaribio ndani ya mwaka mmoja kabla ya kukabidhiwa kwa Serikali Februari 2025.

Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema kuwa bandari hiyo itakuwa na karakana pamoja na sehemu itakayotosha kuegesha meli kumi.

“Bandari hii itakuwa na karakana ambayo itatumika kutengeneza na kukarabati meli…

 Pia bandari itakuwa na uwezo wa kugesha meli kubwa hata kumi kwa wakati mmoja zenye urefu wa mita 30 kutoka kokote duniani,” alisema Waziri Ulega.

Mkoa wa Lindi ni miongoni mwa mikoa maskini nchini licha ya kuwa na rasilimali lukuki ikiwemo bandari na nishati ya gesi.


Soma zaidi


Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inabainisha kuwa Lindi ulikuwa miongoni mwa mikoa mitano nchini yenye kiwango kidogo cha pato halisi la mkoa (Regional GDP per current market prices) ukiwa na pato la Sh3.2 trilioni sawa na asilimia 2.0 ya pato la Taifa.

Mapema Juni mwaka jana Serikali ilisaini mkataba na kampuni ya ujenzi kutoka  China ya China Harbour Engineering Company (CHEC) jijini Dodoma  kujenga bandari hiyo katika Bahari ya Hindi. 

Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa wakati huo Mashimba Ndaki aliwaambia wanahabari kuwa wanatarajia bandari hiyo itavutia zaidi wawekezaji na kutoa ajira kwa wakazi wa mikoa hiyo. 

Rais Samia akiweka jiwe la msingi katika bandari ya uvuvi ya Kilwa Masoko.Picha|Ikulu Mawasiliano/Twitter (X)

Boti za kisasa 160 kutolewa kwa wavuvi

Wakati wakazi wa kusini wakisubiria kukamilika kwa bandari hiyo ili kufaidi fursa za kiuchumi, Serikali imesema imeanza kutoa mikopo ya riba nafuu ya boti za kisasa za uvuvi zitakazosaidia kuongeza mavuno ya samaki. 

Katika mpango huo, Serikali itakopesha boti 160 na vifaa vingine vya uvuvi zikiwemo nyavu, kifaa cha kuongozea boti na vifaa vya kuhifadhia samaki vyenye thamani ya Sh11.5 bilioni. Boti hizo zitagawiwa kwa wavuvi  pamoja na wakulima wa mwani katika bahari ya hindi na maziwa makuu.

Rais Samia amewaambia wakazi wa Kilwa Masoko kuwa anataka kuona boti hizo zikitumika ipasavyo katika kuzalisha ajira na kuongeza kipato cha jamii.

“Boti hizo zitatumika kuzalisha ajira za moja kwa moja zipatazo 3,295 na kukuza kipato cha jamii…na zitarahisisha sulubu kubwa waliokuwa wakipata wavuvi na wakulima wa mwani,” amesema Rais Samia.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

Nukta TV

🔴LIVE: HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA ULINZI NA IKISOMWA BUNGENI

🔴LIVE: HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA ULINZI NA IKISOMWA BUNGENI

Nukta TV

Fahamu kuhusu Virusi vya ‘Hantavirus’ na nini chanzo chake ?

Fahamu kuhusu Virusi vya ‘Hantavirus’ na nini chanzo chake ?

Nukta TV