Tanzania yafikisha watu milioni 61.7

October 31, 2022 1:09 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Hilo ni sawa na ongezeko la asilimia 3.2 ikilinganishwa na idadi ya watu milioni 44.9 waliokuwepo mwaka 2012.

Dar es Salaam. Idadi ya watu Tanzania imefikia milioni 61.7  Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza leo Oktoba 31, 2022 wakati akitoa matokeo ya awali ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 jijini Dodoma.

Hilo ni sawa na ongezeko la asilimia 3.2 ikilinganishwa na idadi ya watu milioni 44.9 waliokuwepo mwaka 2012.

Kati ya watu hao, milioni 59.8 wako Tanzania Bara.

“Kati ya watu milioni 61.7,  wanawake ni milioni 31.6  sawa na asilimia 51,” amesema Rais Samia. 

Kwa mujibu wa Rais Samia, Tanzania Bara ina watu milioni 59.8 kutoka milioni 43.6 waliokuwepo mwaka 2012 huku Zanzibar kwa matokeo ya awali ya Sensa kwa mwaka huu ina watu milioni 1.8.

 

Dar es Salaam kinara kwa watu wengi

Rais Samia aliyekuwa akishangiliwa mara kwa mara na wananchi katika uwanja wa Jamhuri amesema Mkoa wa Dar es Salaam ndiyo unaongoza kuwa na watu wengi Tanzania wanaofikia milioni 5.4 sawa na asilimia 8.7 ya watu wote nchini.

“Na ndiyo maana Dar es Salaam panapotokea upungufu wa kitu chochote, malalamiko yanakuwa makubwa sana kwa sababu watu wengi wapo pale,” amesema Rais.

Mkoa wa pili ni Mwanza wenye watu milioni 3.6 huku Zanzibar, mkoa wenye watu wengi zaidi ni Mjini Magharibi (893,169)   

Zaidi msikilize Rais Samia hapa

                         

Enable Notifications OK No thanks