Tanzania mwenyeji mkutano mkubwa wa Africa Agri Expo 2026

May 18, 2026 9:07 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Utafanyika Septemba 2 na 3 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
  • TAB Group imewaalika wadau wote wenye nia ya kuwa sehemu ya jukwaa hilo kwa kujisajili kupitia tovuti rasmi ya tukio hilo.

Arusha. Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa 10 wa kilimo (Africa Agri Expo 2026) utakaofanyika Septemba 2 na 3 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo unaotarajia kufanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania utawakutanisha washiriki zaidi ya 10,000 kutoka katika sekta mbalimbali kutoka nchi zaidi ya 35 ambapo kampuni ya TAB Group kwa kushirikiana na kampuni ya habari na teknolojia ya Nukta Africa ni miongoni mwa waandaaji.

Tahir Abdul Bari, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya TAB Group amenukuliwa katika taarifa kwa umma iliyotolewa hivi karibuni akisema “Afrika si soko la baadae ni soko la leo” ikiwa ni msisitizo wa kipekee kwa wafanyabiashara wa sekta ya kilimo barani Afrika kulitumia ipasavyo jukwaa hilo kutengeneza mahusiano endelevu yatakayokuza biashara zao kimataifa.

Mkutano huo utafanyika sambamba na maonyesho ya tatu ya Chakula, Mifugo na Ufugaji wa Kuku (The future Food Livestock & Poultry Expo). Picha| Agri Expo/ Instagram.

Agri Expo ni nini?

Agri Expo ni maonesho makubwa na mkutano wa kimataifa wa kilimo unaowakutanisha wadau mbalimbali kujadili na kuonesha teknolojia mbalimbali za kilimo ikiwemo mashine, vifaa vya kisasa, pembejeo pamoja na fursa za biashara na uwekezaji katika sekta hiyo muhimu Afrika.

Mkutano wa mwaka huu utatoa fursa kwa waoneshaji (Exihibitors) kukutana moja kwa moja na maelfu ya wanunuzi, waingizaji bidhaa na wasambazaji, pamoja na maeneo maalum ya kuonesha bidhaa zao na kupata wateja wapya. 

Mbali na maonesho, mkutano huo utachochea mijadala itakayowaleta pamoja wataalamu wa sekta, viongozi wa Serikali na wadau mbalimbali kujadili masuala muhimu yanayoikabili sekta ya kilimo Afrika hivi sasa, ikiwemo mabadiliko ya tabia ya nchi, usalama wa chakula, ufadhili wa sekta ya kilimo na nafasi ya vijana katika kujenga mustakabali wa kilimo Afrika.

Maonesho hayo huzileta pamoja teknolojia rafiki zinazotumika katika kilimo barani Afrika. Picha| Sacco Review.

Ndani ya siku hizo mbili, washiriki na waoneshaji watapata nafasi ya kushuhudia uzinduzi wa bidhaa na maonesho ya moja kwa moja ikiwemo uzalishaji wa mazao, teknolojia za kilimo cha kisasa, mifumo ya umwagiliaji, teknolojia za kuhifadhi mazao baada ya mavuno, pembejeo za kilimo,mashine za kilimo na teknolojia za kidigitali katika kilimo.

Kwa upande mwingine, mkutano huo utafanyika sambamba na maonyesho ya tatu ya a Chakula, Mifugo na Ufugaji wa Kuku (The future Food Livestock & Poultry Expo) ambapo wahudhuriaji watajionea lishe ya mifugo, suluhisho na tiba za mifugo, teknolojia, miundombinu na vifaa vya usindikaji.

Sababu Agri Expo 2026 kufanyikia Tanzania

Hii ni mara ya pili kwa mikutano mikubwa ya kilimo na chakula kufanyikia nchini Tanzania suala linaloendelea kuchochea fursa ya kukua kwa sekta hiyo nchini Tanzania.

Mwaka 2023 Tanzania ilikuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa wa Afrika wa masuala ya chakula na kilimo (AGRF) utakaofanyika Septemba 5 hadi 8 ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Kwa mujibu wa waandaaji, mkutano wa Agri Expo 2026 utafanyika nchini Tanzania kutokana na  uchumi wa kilimo unaokua kwa kasi, ardhi yenye rutuba, na uwekezaji mkubwa wa Serikali katika miundombinu ya kilimo.

TAB Group imewaalika wadau wote wenye nia ya kuwa sehemu ya jukwaa hilo kwa kujisajili kupitia tovuti rasmi ya tukio hilo https://africa-agriexpo.com/aae2026/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
PART 2: Yafahamu magari 10 yanayotumia kiwango kidogo cha mafuta.

PART 2: Yafahamu magari 10 yanayotumia kiwango kidogo cha mafuta.

Nukta TV

🔴LIVE: LIVE:WABUNGE WAKIWACHAPA MASWALI MAWAZIRI | Bunge la 13 | Kikao cha 28

🔴LIVE: LIVE:WABUNGE WAKIWACHAPA MASWALI MAWAZIRI | Bunge la 13 | Kikao cha 28

Nukta TV

PART 1: Yafahamu magari 10 yanayotumia kiwango kidogo cha mafuta

PART 1: Yafahamu magari 10 yanayotumia kiwango kidogo cha mafuta

Nukta TV