Tala haijaondoka Tanzania, imesitisha huduma kujitathmini

September 18, 2019 1:54 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link

Kwa nchi zingine zinazofikiwa na huduma ya Tala zikiwemo Kenya, India, Mexico na Ufilipi, uongozi huo umesema huduma zitaendelea kama kawaida. Picha|Mtandao.


  • Uongozi wa kampuni ya kutoa mikopo kwa njia ya simu ya Tala umesema haujasitisha kutoa huduma hiyo moja kwa moja nchini Tanzania na imeweka bayana kuwa maamuzi hayo hayajafikiwa.
  • Kusitisha kutoa huduma zake Tanzania, ni hatua ya kutathmini mwenendo wa soko. 
  • Tala imetoa mikopo yenye thamani ya  Sh2.3 billioni na kufanikiwa kuwafikia Watanzania  milioni tatu.

Dar es Salaam. Uongozi wa kampuni ya kutoa mikopo kwa njia ya simu ya Tala umesema haujasitisha kutoa huduma hiyo moja kwa moja nchini Tanzania na imeweka bayana kuwa maamuzi hayo hayajafikiwa.

Katika taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo nchini Kenya leo (Septemba 18, 2019), imesema kusitishwa kwa huduma nchini Tanzania ni kwa ajili ya kutathmini muelekeo wa kampuni hiyo baada ya kukamilika kwa kipindi cha majaribio ya utoaji wa huduma hizo za mikopo Tanzania.

“Tala haijafanya maamuzi ya kusitisha shughuli zake moja kwa moja. Baada ya majaribio ya bidhaa yetu nchini Tanzania, tumesitisha kutoa huduma na tunafanya tathmini ya utendaji wetu kuona mwelekeo wetu kimasoko,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.


Zinazohusiana: 


Uongozi wa Tala nchini Kenya umesema hadi sasa Tala imetoa mikopo yenye thamani ya  Sh2.3 bilioni na kufanikiwa kuwafikia Watanzania  milioni tatu.

Kwa nchi zingine zinazofikiwa na huduma ya Tala zikiwemo Kenya, India, Mexico na Ufilipi, uongozi huo umesema huduma zitaendelea kama kawaida.

Enable Notifications OK No thanks