Takukuru Mwanza yaonya rushwa kipindi cha uchaguzi

November 21, 2024 4:18 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Yasema wataotoa na kupokea rushwa wote watachuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Mwanza. Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Mwanza imewaonya wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na uchaguzi mkuu kuacha tabia ya kutoa rushwa kwa wananchi kuwashawishi ili wawachague.

Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mwanza, Idirisa Kisaka aliyekuwa akizungumza na wanahabari leo Novemba 21,2024  amesema taasisi hiyo imejipanga kufuatilia vitendo vyote vya rushwa katika uchaguzi kabla, wakati na baada ya uchaguzi na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria.

“Mara nyingi wagombea wasiokuwa waaminifu wanatumia nafasi hii kuwashawishi wananchi kwa kuwapatia chochote ili wawachague, na pia kuna baadhi ya wananchi ambao nao wanatumia kishawishi kwa wagombea ili wawapatie chochote wote kwa pamoja tunawafuatilia,” amesema Kisaka.

Kisaka ametoa angalizo kwa wananchi kuacha tabia hiyo na kwamba wawachague viongozi ambao ni waadilifu na watoe taarifa pale ambapo wataona kuna viashiria vya wagombea kutoa rushwa.

Pamoja na kuwachukulia hatua Takukuru imejipanga kutoa elimu kwa makundi mbalimbali juu ya  madhara ya rushwa na makosa yatokano na  rushwa katika uchaguzi huo.

Aidha, Takukuru ifanya uchambuzi wa mifumo, kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na kuchunguza makosa ya rushwa kwa mujibu wa sheria.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
27 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
28 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
28 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Nukta TV

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Nukta TV

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Nukta TV