Wanahabari wahimizwa kudhibiti rushwa wakati wa uchaguzi

September 20, 2024 8:05 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Takukuru yasema kudhibiti rushwa kutafanya vyombo vya habari viwe huru.

Arusha. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Arusha imetoa elimu kwa waandishi wa habari juu ya umuhimu wa kudhibiti vitendo vya rushwa vinavyofanyika hususan kabla na wakati wa uchaguzi.

Takukuru imetoa elimu hiyo wakati Tanzania ikijiandaa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwishoni mwa 2024 na ule wa Serikali kuu unaotarajia kufanyika mwakani.

Zawadi Ngailo, Mkuu wa Takukuru Arusha aliyekuwa akizungumza katika semina maalum ya taasisi na wanahabari hiyo leo Septemba 20. 2024 amesema rushwa ikidhibitiwa vyombo vya habari vitaweza kufanya kazi kwa uhuru.

“Kuna wakati kulikuwa na habari za kiuchunguzi sasa hivi zimepungua sana, tukapofanya wajibu wetu kuzuia rushwa katika uchaguzi inamaanisha hata hizi habari zitaanza kuripotiwa…

…Itasaidia kwasababu mtakuwa mnafanya wajibu wa ule muhimili wa nne wa kusimamia,” amesema Ngailo.

Aidha, Ngailo ameyataja madhara mengine ya rushwa wakati wa uchaguzi ikiwemo kuchelewesha shughuli za maendeleo ya jamii zilizopangwa kufanyika kwa kipindi husika.

Enable Notifications OK No thanks