Tahadhari: Mvua kuendelea kunyesha Dar, Pwani, Tanga hadi jumapili

May 10, 2019 2:27 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imewataka wananchi wa mikoa hiyo waendelee kuchukua tahadhari ya uharibifu miundombinu unaoweza kutokea.
  • Mvua hizo zitapungua baada ya jumapili lakini zinaweza kurejea tena kuelekea katikati ya Mei.

Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imewataka wananchi wa mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na visiwa vya Unguja na Pemba waendelea kuchukua tahadhari dhidi ya athari za mvua kubwa katika maeneo yao ambazo zinaweza kuendelea kunyesha hadi katikati ya mwezi Mei mwaka huu.

Athari hizo ni pamoja na uharibifu wa miundombinu ya usafiri zikiwemo barabara na makazi ya watu hasa maeneo ya mabondeni. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo (Mei 10, 2019) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Samwel Mbuya, mvua hizo ambazo zimeendelea kunyesha mfululizo kwa siku kadhaa zilizopita zitaendelea kwa siku mbili zijazo na zitapungua baada ya jumapili ya Mei 12 mwaka huu. 

Hata hivyo amesema viasharia vya hali ya hewa vinaonyesha kuwa mvua hizo zitarejea tena kuelekea katikati ya Mei. 

“Mamla ya hali ya hewa inapenda kutoa taarifa kwamba mvua hizi za mfululizo ambazo zinatokana na kuimarika kwa mvua katika eneo hili la pwani ya kaskazini bado zipo na zitaendelea kwa siku mbili kuanzia hivi sasa,” amesema Mbuya.


TMA imeeleza kuwa  mvua hizo za mfululizo zinazoambatana na vipindi vifupi vya upepo mkali zinatokana na kuimarika kwa ukanda wa mvua katika eneo la pwani ya kaskazini bado zipo na zitaendelea kwa siku mbili kuanzia leo. 


Soma zaidi: 


Kutokana na hali hiyo ya mvua za mfululizo, TMA imewashauri wananchi kuendelea kufuatilia na kuzifanyia kazi taarifa zinazotolewa na mamlaka husika ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza katika maeneo yao.

 

Mvua hizo za masika pia zinaendelea katika maeneo mengine ya nchi yanayopata vipindi viwili vya msimu wa mvua kwa mwaka ikiwemo ukanda wa ziwa Victoria na maeneo ya nyanda za juu mashariki katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na sehemu ya mkoa wa Manyara ambapo  katika maeneo hayo viwango vya mvua ni vya kawaida.  

Baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam yameathirika na mvua hizo ikiwemo eneo la Jangwani ambalo lilipata mafuriko nyakati za asubuhi na kutatiza shughuli za usafiri katika eneo hilo. 

Mathalan,  mabasi yaendayo haraka yalisitisha safari zake katika barabara ya Magomeni hadi Faya inayokatiza Jangwani kabla ya kuruhusiwa tena mchana wa leo.

 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
21 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
21 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
21 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Nukta TV

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Nukta TV

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

Nukta TV