July 14, 2026 9:30 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Dola ya Marekani imeendelea kuuzwa na kununuliwa kwa bei sawa na jana huku sarafu nyingine zikionyesha mabadadiliko madogo.

Dar es Salaam. Soko la fedha za kigeni limeendelea kuonyesha utulivu leo Julai, 14, 2026 huku baadhi ya sarafu zikionesha mabadiliko madogo katika benki za biashara nchini.

Takwimu za viwango vya kubadili fedha katika benki za CRDB na NMB zinaonyesha kuwa Dola ya Marekani imeendelea kuuzwa kwa Sh2,675 na kununuliwa kwa Sh2,595 kiwango sawa na kilichotumika jana Julai 13, 2026.

Hii inamaanisha kuwa Watanzania na wafanyabiashara wanaotumia Dola katika miamala yao wataendelea kutumia kiwango kile kile ambacho walitumia jana hali inayoleta utulivu wa kasi ya mfumuko wa bei katika soko hilo.

Kwa upande wa Pauni ya Uingereza imeonesha mabadiliko madogo ikishuka kiduchu katika benki zote mbili ambapo katika benki ya CRDB bei ya kununua imeshuka kwa Sh4.53 kutoka Sh3,374.17 iliyotumika jana hadi Sh3,369.64 leo huku bei ya kuuza ikishuka kutoka Sh3,674.17 hadi Sh3,669.17 sawa na punguzo la Sh6.

Katika benki ya NMB, Pauni ya Uingereza, imenunuliwa kwa Sh3,337 hii leo ikilinganishwa na Sh3,343 ya jana, ikiwa ni sawa na kushuka kwa Sh6, na wakati huo bei ya kuuza pia imeshuka kutoka Sh3,688 hadi Sh3,682, ikiwa ni sawa na punguzo la Shilingi 6. 

Kwa upande wa sarafu za kikanda Shilingi ya Kenya na Uganda zimeendelea kuonyesha utulivu zikionyesha mabadiliko madogo dhidi ya Shilingi ya Tanzania.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
25 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Elimu ya kodi mwarobaini wa wafanyabiashara kuikwepa TRA, ianzie shuleni

Elimu ya kodi mwarobaini wa wafanyabiashara kuikwepa TRA, ianzie shuleni

Nukta TV

Rais Samia: Serikali chini ya Magufuli haikutaka kuyumbishwa kukamili kwa JNHPP

Rais Samia: Serikali chini ya Magufuli haikutaka kuyumbishwa kukamili kwa JNHPP

Nukta TV

Rais Samia: Umeme wa SGR hautoingiliwa, Dodoma umeme uhakika 24/7

Rais Samia: Umeme wa SGR hautoingiliwa, Dodoma umeme uhakika 24/7

Nukta TV