Simu unazoweza kununua kwa bei chini ya Sh1 milioni

November 4, 2020 12:55 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pamoja na simu za iPhone, Samsung na Google Pixel.
  • Simu hizi zinatofautina uwezo wa uhifadhi, kamera na hata skrini.
  • Endapo unahitaji simu yenye uwezo zaidi, bado yapo machaguo lukuki mtandaoni.

Dar es Salaam. Unafikiria simu gani unaposikia neno simu nzuri? Baadhi ya watu hufikiri kuwa simu nzuri ni zile zinazogharimu mamilioni ya fedha huku sifa kuu za simu hizo zikiwa ni kamera nzuri, muonekano na uwezo mkubwa wa utendaji kazi.

Hata hivyo, kama mfuko wako hauruhusu kutoa fedha zaidi ya Sh1 milioni kununua simu yako ya mkononi, bado una nafasi ya kupata simu nzuri yenye vitu unavyovitaka kwa fedha uliyonayo.

Shirika la habari la The verge limeorodhesha simu nzuri zaidi za mwaka 2020 zinazopatikana kwa bei chini ya Sh1 milioni kwa mahitaji ya kamera na hata skrini kubwa. Ni simu gani hizo?

iPhone SE

Kwa mujibu wa The Verge, simu hii imeshinda kipengele cha simu janja bora kuliko zote zinazouzwa chini ya Sh1.6 milioni (Dola 500 za Kimarekani)

Kama unahitaji simu ambayo ina uwezo mzuri wa kamera, kasi katika utendaji kazi, na betri lenye kukidhi matumizi ya simu janja, unaweza kupepesa jicho lako kwenye simu hii ambayo inapatikana kwa Sh925,300

Kwa pesa hiyo utapata simu hiyo yenye uwezo wa uhifadhi wa GB64, kamera yenye megapikseli 12 (MP12) na kasi ya utendaji kazi kama uliopo kwenye simu za iPhone11.

Google Pixel 4A

Kama unatafuta simu yenye kamera bora kwa bei chini ya Sh1 milioni, safari yako inaweza kuwa imefikia kikomo.

Simu hii imezinduliwa rasmi Agosti 2020 nchini Marekani huku kamera yake ndiyo ikiwa kitu kinachoitofautisha na simu zote unazoweza kuzipata kwa gharama nafuu.

Kama wewe ni mpenzi wa Android  Pixel 4A ni simu ambayo kamera yake ina uwezo wa MP12 kukupatia picha na video nzuri sawa na wale wenye simu za Sh3.5 milioni.

Ikilinganishwa na iPhone SE, simu hii inatoa picha nzuri zaidi inauzwa kwa Sh809,331 tu.

SamsungGalaxy A51

Endapo kiu yako ni simu yenye skrini kubwa, utafutaji wako umefika mwisho.

Skrini ya simu hii ina ukubwa wa inchi 6.5 huku ikiambatana na uwezo wa uhifadhi wa GB128 na betri lenye uwezo wa kuhifadhi chaji kwa siku nzima ikitegemea na matumizi yako.

Pia, simu hii iko nyuma kwa picha ikilinganishwa na Pixel 4A lakini ina leni za kamera nyingi hivyo kukupa uwezo wa kupiga picha kwa mapana zaidi kuliko zingine huku bei yake ikiwa 924,617.


Soma zaidi


Moto G Power

Kama shida yako ni betri ya simu, tiba imepatikana.

Simu hii ambayo betri lake limeyapiga kikumbo mabetri ya simu lukuki zinazouzwa kwa bei chini ya Sh1 milioni inaambatana na betri lenye uwezo wa kuhifadhi chaji (mAh) yenye ukubwa wa mAh5,000 na kukuwezesha kutumia kwa siku mbili hadi siku tatu.

Changamoto yake ni kuwa uhifadhi wake ni wa GB 64 tu na kamera yake ikitosheleza matumizi ya picha za kutuma WhatsApp status na mitandao mingine ya kijamii ikiwa na ukubwa wa MP16.

Hata hivyo, endapo simu hizi bado hazijafikia matarajio yako, bado kuna simu nyingi ambazo unaweza kuangazia zikiwemo Huawei Honor 10X 6/128Gb inayouzwa kwa Sh753,675.

Enable Notifications OK No thanks