Siku ya Mazingira duniani kufanyika kwa namna yake Tanzania

May 27, 2024 3:00 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Itapambwa na shughuli mbalimbali ikiwemo usafi utakaofanyika nchi nzima na kuongozwa na viongozi mbalimbali akiwemo Dk Philip Mpango.

Dar es Salaam. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Selemani Jafo amesema maadhimisho ya siku ya mazingira duniani nchini Tanzania yatafanyika katika ngazi ya kitaifa na mikoa kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo usafi.

Jafo aliyekuwa akizungumza na wanahabari leo Mei 27, 2024 jijini Dar es Salaam amesema kilele cha maadhimisho hayo kitakuwa Juni 5, 2024  mkoani Dodoma ambapo Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

“Katika hafla hiyo mgeni rasmi atagawa vyeti vya kutambua makampuni yaliyofanya vizuri katika eneo hilo (la usimamizi wa mazingira) pia atazindua Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu ya mwaka 2024 ,” amesema Waziri Jafo.

Uzinduzi wa maadhimisho hayo utafanyika  Mei 29, 2024 mkoani Katavi ambapo pamoja na mambo mengine Waziri Jafo atakayekuwa mgeni rasmi atazindua mradi wa urejeshwaji uoto wa asili unaotekelezwa katika wilaya saba mkoani humo, mabwawa ya kunywesha mifugo pamoja na ugawaji wa hati 4,450.

“Shughuli nyingine zitakazozinduliwa ni pamoja na josho la mifugo, banio pamoja na birika la kunyweshea maji mifugo yetu ambapo ngombe mbuzi watapata nafasi ya kunywa maji,” ameongeza Jafo.

Baada ya shughuli hiyo, Serikali chini ya Baraza la Mazingira (NEMC) itafanya kongamano la mazingira katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es es Salaam ambapo Makamu wa Rais Dk Philip Mpango atalifungua rasmi.


Soma zaidi:Rais Samia: Baraza la Amani na Usalama la AU limetusaida kukabiliana na ugaidi Afrika


Miongoni mwa washiriki wa kongamano hilo ni pamoja na wadau wa mazingira, taasisi za kiserikali, sekta binafsi, mashirika ya kimataifa, asasi za kiraia, taasisi za kielimu na taasisi za kitafiti.

“Sisi tunaamini kuwa ni kongamano muhimu sana…wadau watapata fursa ya kujadili mada adhimu zinazohusu changamoto za utunzaji wa mazingira na kutoa muelekeo wa hatua muhimu zinazopaswa kuchukuliwa,” amesema Jafo.

Dk Mpango, Majaliwa, Dk Tulia  kuongoza usafi Tanzania

Jafo amesema Dk. Mpango atawaongoza wananchi na viongozi wengine kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ikiwemo fukwe za Coco beach.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ataongoza usafi katika mkoa wa Geita ambapo miongoni mwa maeneo yatakayopitiwa ni Wilaya ya Chato, wakati huo mkoani Dodoma Naibu Waziri Mkuu Dotto Biteko ataongoza shughuli hizo lengo likiwa ni kuweka maeneo yote safi.

Shamra shamra hizo za usafi pia zitaendelea katika jiji la Mbeya zikiongozwa na Spika wa Bunge na Rais wa Mabunge Duniani (IPU) Dk. Tulia Ackson huku Jaji Mkuu wa Tanzania Dk. Ibrahim Juma akiwaongoza watu wa mkoani Arusha huku mikoa ya Kigoma na Lindi ikiongozwa na wakuu wa mikoa hiyo. 

Maadhimisho hayo yatatamatishwa na maonesho ya mazingira katika ukumbi wa Jakaya Kikwete (JKCC) mkoani Dodoma kuanzia Juni 1 hadi 5 mwaka huu.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
17 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
17 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
17 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Nukta TV

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Nukta TV

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Nukta TV