SI KWELI: TEC Yatoa Waraka wa Kusomwa kwa Wiki 10 Mfululizo Katika Parokia Zote

May 3, 2025 4:40 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link

Dar es Salaam. Kumekuwa na waraka unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii na majukwaa mbalimbali ya kidijitali, ukidaiwa kuwa umetolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC). Waraka huo unatoa agizo kwamba usomwe katika parokia zote, vigango, na jumuiya ndogondogo kwa muda wa wiki 10 mfululizo.

Waraka huo una kichwa cha habari: “WARAKA WA KICHUNGAJI KUSOMA KATIKA PAROKIA ZOTE, VIGANGO, NA JUMUIYA NDOGO NDOGO ZOTE NCHINI TANZANIA KWA WEEK 10 MFULULIZO.”

Taarifa hii imezua taharuki miongoni mwa waumini na wananchi kwa ujumla, ikiwafanya wengine kuhoji msimamo wa Kanisa Katoliki kuhusu masuala ya kijamii na kisiasa nchini.

UKWELI: Waraka huo ni feki, TEC yakanusha vikali

Nukta Fakti, kupitia uchunguzi wake, imebaini kuwa waraka huo ni wa kughushi na haujatolewa rasmi na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).

Kupitia tamko lao rasmi, TEC imekanusha vikali kuwepo kwa waraka huo na imetoa rai kwa waamini pamoja na Watanzania wote kupuuza taarifa hizo zisizo za kweli.

Katika taarifa hiyo, TEC imesema: “Tunapenda kuwatangazia waamini na Watanzania wote kwa ujumla, kupuuza kabisa waraka huo ambao haukutolewa na Baraza la Maaskofu, na usio na maslahi yoyote kwa nchi yetu.”

Aidha, uchunguzi umebaini kuwa aina ya mwandiko (font) uliotumika katika waraka huo si ile inayotumika katika nyaraka rasmi za TEC, jambo linaloendelea kuthibitisha kuwa waraka huo umetengenezwa na watu wasiokuwa na mamlaka wala uhusiano wowote rasmi na baraza hilo.

TEC pia imetoa wito kwa waamini na watu wote wenye mapenzi mema kutojihusisha na taarifa au vitendo vyovyote vinavyoweza kuhatarisha amani, mshikamano na upendo miongoni mwa Watanzania.

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...

Enable Notifications OK No thanks