Si kweli: Chadema imemfuta uanachama John Mrema

April 8, 2025 4:42 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Chadema imewataka wananchi kuipuza taarifa hiyo ya upotoshaji.

Dar es Salaam. Huenda wewe ni miongoni mwa watu waliokutana na taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii, hususan mtandao wa X (zamani Twitter) zikidai kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemfuta uanachama mwanachama wake John Mrema. Habari hiyo si ya kweli na unapaswa kuipuuza.

Taarifa hii ya upotoshaji imesambaa ikionekanama kama tamko rasmi lililoandikwa na Chadema likiwa na mhuri pamoja na sahihi ya Afisa Habari wa chama hicho Brenda Rupia imeeleza kuwa Chadema imefikia hatua ya kumfuta uanachama John Mrema baada ya kugundua kuwa hana nia njema na chama hicho. 

“Hatua hii imefikiwa baada ya kubaini kwamba Bw. John Mrema na kundi lake linalojiita G55 hawana nia njema na mustakabari wa Chama na wana malengo yakudhoofisha maazimio kadhaa yaliyopitishwa” inasomeka taarifa hiyo.

Aidha taarifa hiyo imeendelea kwa kueleza kuwa uamuzi huo wa Chadema umefikiwa na baada ya Kamati Kuu ya Chama hicho kukutana kwa dharura na kujadiliana mambo kadhaa ikiwemo oparesheni inayoendelea ya Chama hiko ya ‘No Reform, No Election’.

Hata hivyo Afisa Habari wa Chama hicho amekanusha taarifa hizo na kusema kuwa taarifa hizo si za kweli na hivyo zinapaswa kupuuzwa.

Kupitia kurasa rasmi za Brenda Rupia, taarifa hizo hazina ukweli wowote na anaomba zipuuzwe kwani kamati kuu haijakaa kikao chochote, akisisitiza kuwa wenye mamlaka ya kumfuta uanachama John Mrema kwa sasa ni wajumbe katika tawi lake la chama lililopo Segerea. 

“Kamati haijakaa popote, wajumbe wa kamati kuu wengi wapo field akiwemo Mwenyekiti wa Chama Taifa, Katibu Mkuu wa Chama Taifa…na hizo ni taarifa za uongo na naomba zipuuzwe” amesisitiza Rupia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Enable Notifications OK No thanks