Sh307 milioni zawaweka matatani watendaji 34 Kagera

June 23, 2020 1:04 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Maafisa wanne wamesimamishwa kazi huku Watendaji 30 wakikabidhiwa mikononi mwaka polisi na TAKUKURU.
  • Wameshindwa kurejesha Sh307 milioni za mapato ya Halmashauri ya Biharamulo.

Dar es Salaam. Watumishi 30 katika Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo wakiwemo watendaji wa vijiji na kata leo wamekabidhiwa mikononi mwa polisi kwa kushindwa kurejesha Sh307 milioni zilizokusanywa kutoka vyanzo vya mapato ya ndani bila kupelekwa benki.

Mkuu wa mkoa huo Brigedia Jenerali Marco Gaguti amemwagiza Kamanda wa Polisi mkoani humo pamoja na Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuwakamata watendaji hao mara moja ili wakajibu tuhuma zinazowakabili.

“Nilikuja hapa nikatoa maelekezo kwa wale wote waliokuwa wanakusanya fedha kwa kutumia mashine za “Poss” bila kuzipeleka benki kuwa warejeshe fedha na nikawapa siku saba lakini fedha iliyorejeshwa ni asilimia 2.

“Hapa nina orodha ya watendaji 30 ambayo nampatia kamanda wa polisi kuhakikisha watu hao wanakamatwa popote walipo na wengine wanne hawa naagiza wasimamishwe kazi lakini wawe chini ya uangalizi wa kamati ya ulinzi na usalama ili kutoa ushirikiano,” amesema Brigedia Jenerali Gaguti leo Juni 23, 2020 wilayani humo.

Watumishi wa halmashauri hiyo waliosimamishwa kazi ni pamoja na aliyekuwa  Kaimu mweka hazina Sospiter Makene, Maafisa Tehama Jastine Banula na Rogers Semukoko na Afisa Biashara Beatrice Gurusya


Zinazohusiana


Amesema watumishi wa umma wanatakiwa kuwa waadilifu na kuiogopa fedha ya Serikali na kuahidi kuwachukulia hatua wote watakaobainika wakifanya vitendo vya ubadhilifu na kutoa onyo kali kwa watendaji wa vijiji na kata mkoani humo kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa mapato ya serikali bila kuleta “ujanja ujanja”.

Ikumbukwe kuwa, Gaguti amechukua uamuzi huo baada ya kutoa siku saba kwa watumishi hao kurejesha fedha hizo kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo kilichofanyika Juni 5, 2020 mwaka huu kilichokuwa kina lengo la kujibu hoja za Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV