Serikali yaingilia kati sakata la madereva wa malori kugoma

July 26, 2022 2:08 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link

Pichani, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongoza kikao kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma. Kushoto kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene na kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka. Picha| Ofisi ya Waziri Mkuu.


  • Yawataka waajiri kuwapa stahiki zao.
  • Yasema wanaogoma watachukuliwa hatua.
  • Yakaribisha mazungumzo kumaliza mgogoro wa madereva na waajiri.

Dar es Salaam. Kufutia sakata la madereva wa malori nchini  kutishia kugoma kwa kile walichodai kutotimiziwa maslahi yao, Serikali imesema itahakikisha inaendelea kusimamia madai ya madereva pamoja na haki za waajiri katika kutekeleza madai ya madereva wa malori.

Waziri mkuu Kassim Majaliwa aliyekuwa akizungumza kwenye kikao na mawaziri na manaibu waziri wa wizara mbalimbali jijini  Dodoma leo Julai 26 amesema lengo  la serikali ni kuhakikisha madereva wanaendelea na ajira zao na wanapata maslahi yao kwa mujibu wa sheria ili waweze kuendesha shughuli zao na familia zao. 

“Serikali itasimamia madai ya madereva  na haki za waajiri, katika kutekeleza madai ya madereva wasije wakawajibika na vitu ambavyo haviko kwenye sheria zetu za nchi,” amesema Majaliwa.

Aidha, Majaliwa amekitaka Chama Cha Madereva nchini kiruhusu huduma za usafirishaji ziendelee kutolewa wakati Serikali ikiendelea kushughulikia masuala yao.

“Serikali haitaridhika kuona madereva wanalalamika kila siku na pia si vizuri waajiri wakabebeshwa mizigo iliyo nje ya sheria,” amesema Mjaliwa.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Innocent Bashungwa, 

Mawaziri wengine waliohuria ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara hizo na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Camilius Wambura ambapo pamoja na mambo mengine kikao hicho kililenga kujadili suala la mgomo wa madereva.


Kiini cha mgomo vyatajwa

Majaliwa amesema malalamiko ya madereva hao ni kutopewa mikataba ya kazi, kutokuwa na uhakika wa matibabu yao na familia zao (bima ya afya) na kutounganishwa katika mifuko ya hifadhi ya jamii ili wawe na uhakika wa kupata mafao baada ya kustaafu. Pia kutopatiwa posho mbalimbali.

Waziri Mkuu amesema madereva hao wanataka kupokelea mishahara yao benki badala ya kupewa mikononi.

“Chama cha madereva kiorodheshe kampuni ambazo hazijatekeleza makubaliano baina yao na madereva badala ya kuzuia malori kutoa huduma kwani  kufanya hivyo ni uhujumu uchumi,” amesisitiza Majaliwa.

 Amesema Serikali haipendi kuona mgogoro huo ukiendelea na kuathiri shughuli za waajiri ambao wametekeleza majukumu yao, hivyo ameiagiza Wizara ya Mambo ya Ndani iondoe vikundi vinavyozuia madereva hao kutekeleza majukumu yao. 

“Kama kuna dereva ambaye hajakubaliana na kampuni yake atoe taarifa kwenye chama chao na kifanye jitihada za kutatua jambo hilo na iwapo chama hicho kitashindwa kitoe taarifa Serikalini ili isaidie katika kusimamia madai yao ikiwa ni pamoja na kuona wanachodai na kumsikiliza anayedaiwa kisha kufanya maamuzi,” amesema. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
7 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
7 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV