Serikali yaanika mafanikio 10 uwekezaji wa kampuni ya Dp World bandari ya Dar es Salaam

November 1, 2024 4:32 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pamoja na kuanzishwa kwa miradi mipya ya uwekezaji.
  • Mapato yaTRA kuongezeka hadi kufikia Sh1 trilioni.

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imesema uwekezaji uliofanywa na kampuni ya Dp World katika bandari ya Dar es Salaam umechangia ukuaji wa biashara na ukusanyaji wa mapato unaofanyika katika bandari hiyo. 

Mafaniko hayo yatokanayo na kampuni ya Dp World yanakuja ikiwa ni miezi mitano tangu kampuni hiyo ianze utekelezaji wa shughuli zake katika bandari ya Dar es Salaam Aprili 15 mwaka huu.

Oktoba 22, 2023 Serikali ilisaini mikataba mitatu ya uwekezaji na kampuni ya Dp word  uliohusisha uendeshaji wa bandari katika uhudumiaji wa makasha, mzigo mchanganyiko na shehena ya magari hatua iliyopigwa vita na wanaharakati na baadhi ya wanasiasa nchini.

Waziri wa Mipango na Uwekezaji Prof Kitila Mkumbo aliyekuwa akiwakilisha mapendekezo ya mpango wa Taifa wa maendeleo unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali mwaka 2025/2026 leo Novemba 1,2024 Bungeni jijini Dodoma amesema uwekezaji huo umesaidia kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato bandarini.

“Kuongezeka kwa mapato ya kodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hadi kufikia Sh1 trilioni Septemba 2024 ukilinganisha na wastani wa Sh850 bilioni kwa mwezi hiii imetokana na TRA kuweza kuchakata mizigo mingi zaidi na kwa muda mfupi,” amesisitiza Prof Mkumbo.

Prof Kitila ameyataja mafanikio mengine ya uwekezaji wa kampuni hiyo nchini kuwa ni pamoja na kupungua kwa muda wa meli kusubiri nangani.

Picha ya hii inanosha namna mizigo inavyopakuliwa bandarini. Picha/ Dp World.

Kutoka wa siku 46 kwa mwezi Mei 2024 hadi kufikia wastani wa siku saba ikiwa ni sawa na siku sifuri kwa meli za makasha siku 12 kwa meli za kichere na siku 10 kwa meli za mizigo mchanganyiko.

Hatua hiyo imetokana na kampuni hiyo kufunga vitendea kazi vya kisasa vya SSG na RTG vinavyosaidia kupunguza muda wa kupakia na kushusha kwa mizigo.

“Muda wa kuhudumia meli za makasha getini umepungua kutoka wastani wa siku saba hadi wastani wa siku tatu hivyo kupunguza idadi ya meli zinasubiri angani kutoka wastani wa meli 35 Septemba 2023 hadi meli 15 Septemba 2024,” amesema Prof Mkumbo.

Uwepo wa Dp Word umeongeza shehena zinazohudumia kutoka shehena 141,889 Mei 2024 kufikia shehena 168,331 Septemba ikiwa ni ongezeko la asilimia 18 katika miezi mitano.

Mafanikio mengine nikupungua kwa gharama za uendeshaji  hadi kufikia asilimia 2.7 ya makusanyo wakati ambapo matumizi yalikuwa yakiongezeka kwa asilimia 15.1 kwa mwezi kabla ya kukabidhiwa kampuni hiyo uendeshaji pamoja na kuongezeka kwa shehena zinazohudumiwa kutoka shehena 141,889 Mei 2024 kufikia shehena 168,331 Septemba.

Aidha, mkataba kati ya Serikali na Dp World umesaidia ukusanyaji wa Sh525.3 bilioni ikiwa ni mapato ya shughuli za uendeshaji huku uwekezaji ukiongezeka hadi Sh1.92 trilion.

Kwa upande wa makasha Prof Mkumbo amesema yameongezeka kutoka wastani wa makasha elfu 12,000 kwa mwezi hadi kufikia idadi ya makasha elfu 27,000 mwezi Septemba 2024, idadi hii ya makasha ilikuwa haijawahi kufikiwa katika historia ya bandari ya Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Enable Notifications OK No thanks