Serikali kutatua migogoro ya ardhi inayomilikiwa na madhehebu ya dini

May 17, 2021 6:26 am · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni maeneo yanayomilikiwa na madhehebu yaliyovamiwa na watu.
  • Serikali yasema itaingilia kati.ili kutafuta muafaka.

Mwanza. Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango ameahidi kutatua migogoro mbalimbali ya ardhi inayohusisha maeneo yanayomilikiwa na madhehebu ya dini yakiwemo makanisa yaliyovamiwa na watu. 

 Dk Mpango amaliyekuwa akizungumza Mei 16, 2021 jijini Mwanza katika ibada maalum ya kumsimika Askofu wa  Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Victoria Nyanza, Zephania Ntuza amesema atamtuma Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kushughulikia suala hilo.

Dk Mpango amesema amesikia suala hilo na kwamba kanisa la Anglikana liandike barua rasmi ili kutafuta ufumbuzi kwa taasisi za dini kuvamiwa.

”Hili suala nimesikia na naomba kama kanisa mlilete kwa maandishi ili tuweze kulishughulikia na kulipatia ufumbuzi,” amesema

Kuhusu migogoro katika makanisa mbalimbali hapa nchini, Dk Mpango ameeleza kuwa suala hilo linawakatisha tamaa waumini na kuwarudisha nyuma kiroho na kuhatarisha amani ya nchi.

Kwa mujibu wa Dk Mpango, Serikali inapenda kuona taasisi za dini zinaongozwa kwa kufuata taratibu na kanuni walizojiwekea ili kuepuka migogoro mbalimbali.

“Tumechoka  kusikia migogoro hiyo ambayo  inakatisha tamaa na kurudisha nyuma waumini kiimani, kuwagawa na kushindwa kutekeleza mambo ya kuwajenga kiroho,” amesema Dk Mpango.


Zinazohusiana: 


Awali  Askofu mpya wa kanisa hilo Dayosisi ya Victoria ya Nyanza, aliomba Serikali kusaidia kurejesha  maeneo ya kanisa yaliyovamiwa  katika sehemu mbalimbali nchini.

”Niombe kwa ruhusa yako Mheshimiwa Makamu wa Rais,  Serikali itusaidie ili kurejesha maeneo yetu yaliyovamiwa na ikikupendeza tutayaleta haya kwako kwa  maandishi,” amesema Askofu huyo.

Sherehe hizo za kumsimika askofu huyo zilifanyika katika kanisa la Nicolaus Dayosisi ya Victoria ya Nyanza na kuhudhuriwa na waumini, maaskofu na viongozi wa Serikali kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.

Enable Notifications OK No thanks